Home Habari za michezo NANI BORA KATI YA MANULA NA DIARRA…? KASEJA KAFUMBA MACHO AKISHA KAMTAJA...

NANI BORA KATI YA MANULA NA DIARRA…? KASEJA KAFUMBA MACHO AKISHA KAMTAJA HUYU…

Habari za Michezo

KIPA na kocha wa makipa nchini, Juma Kaseja amewataka makipa kufanya zaidi mazoezi uwanjani kuliko kushinda mitandaoni kuangalia mazoezi na kwamba kwasasa nchini kipa wa Yanga, Djigui Diarra ni bora zaidi.

Msimu uliopita, Diarra ndiye alikuwa kipa bora wa Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) huku akiisaidia timu yake kufika hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kaseja aliyazungumza hayo katika mahojiano maalumu  jijini Dar es Salaam kuwa kwasasa Diarra ndiye bora ingawa kuna wengine wakijitoa zaidi wanaweza kufanya vizuri.

“Ubora wake uko juu, na mpira wa sasa ni wa kisasa unahitaji kipa anayeweza kucheza kwa miguu na mikono, ndiyo maana inatoa picha halisi ya kuona Diarra ana uwezo mkubwa na bora kwasasa,” alisema Kaseja.

Akifafanua juu ya matumizi ya mitandao kipa huyo mkongwe aliyewahi kuzichezea timu mbalimbali ikwemo Simba na Yanga, alisema vijana wengi kwasasa wanaharibiwa na mitandao kwa kufanya mazoezi yanayowekwa mitandaoni na kuona kazi ya ukipa ni nyepesi.

“Utandawazi ni mzuri ila kuna nafasi umewaharibu watu, kuna vijana wanaamini wakiingia YouTube wakiona wanavyofanya mazoezi makipa basi wanadhani nao wanaweza kufanya vile.

“Kuna wadogo wetu wanaamini ukifanya vile unaweza kuwa bora lakini ni kwamba mitandaoni hawawezi kukuwekea kila kitu, ile ni elimu hawawezi kutoa elimu bure maana nao wanalipia kwa kwenda shule kujifunza, huko wanaweka vitu vya sekunde tu ambavyo havikufundishi.

“Anaweka kidogo ili uone apate watu, rai yangu watoke kwenye mitandao waingie viwanjani, wafanye mazoezi, mazoezi ya makipa ni magumu sana na yanahitahi muda, watambue na kuheshimu hiyo nafasi kwa kuipa muda wa ziada wa kufanya mazoezi,” alisema Kaseja

SOMA NA HII  TETESI ZA USAJILI: KUHUSU ISHU YA KUTAKIWA SIMBA...NASHON AANIKA MCHONGO WOTE JINSI ULIVYO...