Home Habari za michezo HATIMAYE ZIMBWE Jr AANIKA ‘KIZIZI CHAKE’ KINACHOMPA NAMBA SIMBA…

HATIMAYE ZIMBWE Jr AANIKA ‘KIZIZI CHAKE’ KINACHOMPA NAMBA SIMBA…

Habari za Simba

Beki wa Kushoto na Nahodha Msaidizi wa Simba SC Mohamed Hussein Zimbwe Jr, ameweka wazi kuwa kikubwa ambacho kinamfanya awe bora ni juhudi pamoja na ushirikiano ndani ya timu.

Beki huyo mzawa yupo kwenye orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya beki bora wa msimu wa 2022/23 akiwa kwenye fungu moja na Henock Inonga Baka, Shomari Kapombe wote wa Simba.

Kwa upande wa nyota kutoka Young Africans ni Bakari Mwamnyeto na Dickson Job nao wapo kwenye kuwania tuzo ya beki bora.

Simba SC ikiwa imefunga jumla ya mabao 66 nahodha huyo msaidizi wa Simba SC, ikiwa ni moja alimpa mshikaji wake Inonga kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar.

Beki huyo amesema: “Kila siku tunafanya kazi kubwa kwenye kusaka ushindi na kinachofanya nizidi kuwa bora ni juhudi na kujituma bila kukata tamaa.

“Pia ninamshukuru Mungu pamoja na familia yangu ambayo imekuwa ikiniombea hivyo bado kuna kazi kubwa ya kufanya kufikia mafanikio.”

SOMA NA HII  KUELEKEA TUZO ZA CAF LEO...PAPE SAKHO HUYU HAPA....MSENEGAL ANAYEIWAKILISHA TANZANIA NA SIMBA KIMATAIFA...