Tetesi za Usajili Simba
Habari za michezo

BAADA YA KUTEMWA SIMBA….GADIEL MICHAEL KUENDA HUKU KUPIGA PESA….

admin July 4, 2023 8:17 pm

Baada ya kutemwa na Simba, mlinzi wa kushoto Gadiel Michael, yuko mbioni kujiunga na klabu ya Singida Fountain Gate Fc ya mkoani Singida.

Gadiel alikuwa sehemu ya kikosi cha Simba kwa misimu minne, mabosi wa Simba wakaachana nae baada ya mkataba wake kumalizika msimu huu.

Singida Fountain Gate pia inatajwa kumsajili mlinda lango Beno Kakolanya ambaye pia ameachwa na Simba baada ya mkataba wake kumalizika.

Matajiri hao wa Singida pia wanatajwa kumuwania beki Kennedy Juma ambaye hata hivyo Simba haina mpango wa kumuacha kwa kuwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja

Zipo taarifa kuwa Kennedy kama ilivyo kwa Joash Onyango, nae aliomba kuachwa ili akajiunge na timu ambayo itampa uhakika wa kucheza.

Kennedy ni miongoni nmwa wachezaji ambao Kocha Robertinho Oliveira alipendekeza kuendelea nao.

‘THANK YOU’ KUZIDI KUSHUKA YANGA…WANAOFUATA NI HAWA… ‘BEKI LA CHAN’ NA YANGA NI SUALA LA MUDA TU….MWENYEWE AANIKA A-Z ISHU ILIVYOPIGWA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply