Habari za Yanga SC
Habari za michezo

BAADA YA DILI LA KUSEPA KUFELI…SHABANI DJUMA AFUNGUKA YANGA WANACHOWAFANYIA WACHEZAJI WA KICONGO

admin July 6, 2023 3:26 am

Mchezaji wa Yanga Djuma Shabani, ambaye ana mkataba na timu hiyo mpaka 2024, amesema ana furaha sana kucheza soka la Tanzania kwa sababu viongozi wa soka wanajua kuwahudumia vyema wachezaji.

Djuma Shabani amezungumza na mwanahabari wa umoja wa wachezaji wa Congo Ufs, Olivier Sefu na kumwambia wachezaji wa Kitanzania hawana matamanio tena ya kuja kucheza Congo DR kama enzi za Mbwana Ally Sammata.

Amesema ligi ya Congo- DR inatia hofu kwa sababu inakosa wasimamizi makini na uratibu mzuri wa ligi huku wachezaji wakipitia kipindi kigumu na kusema kama hawatabadilika basi wasiwe na matumaini yoyote.

Amesema Tanzania ligi haisimami hovyo kama Congo ambako amesema viongozi wana vipaumbele vyao na wala hawachukuliwi hatua huku akipigilia msumari kuwa Tanzania kila klabu inanufaika na haki za matangazo ya televisheni na akiisifu ligi ya Tanzania kuwa na hadhi ya juu kwa kushika nafasi ya 5.

YANGA WAPEWA MASHABIKI 30,000 WA KUNUNU JEZI ZAO MALAWI…RAIS SAMIA ATIA BARAKA… KUHUSU NAMBA 6 MPYA WA YANGA…ALLY KAMWE AANIKA A-Z DILI LILIVYO….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply