Tetesi za Usajili Yanga
Habari za michezo

WAKATI ISHU YA MAYELE IKIWA KIZUNGUMKUTI….MPOLE ANUKIA YANGA…AKUTANA NA MABOSI KUYAJENGA…

admin July 10, 2023 6:45 pm

Mshambuliaji wa FC Lupopo ya DR Congo, George Mpole ameamua kubadili gia akiwa angani, licha ya kuwa alishakubaliana kila kitu na klabu ya Kitayosce ila sasa akili yake ipo Jangwani.

Siku ya Alhamisi alionekana na Bosi Mkubwa wa klabu ya Yanga huku akionekana mwenye furaha.

Huenda akawa mbadala na Hafiz Konkon ambaye Yanga SC wanazungumzwa kumtaka na huenda wakaamua kuachana nae.

Pia kutua kwa Mpole Yanga Sc inaonyesha kuna mshambuliaji mzawa ataondolewa pale, iwe kutolewa kwa mkopo ama kuvunjiwa Mkataba.

George Mpole kabla ya kwenda zake Congo alikuwa mfungaji Bora wa Ligi Kuu kwa msimu wa 2021/22 amabpo alimfunika Mayele kwa kumzidi goli moja.

Washambuliaji wa kati (Mambo yakikaa sawa)

Fiston Mayele

Clement Mzize

Kennedy Musonda

Yusuph Athuman

George Mpole

BAADA YA TETESI ZA KUSEPA KWAKE KUZAGAA LEO….CEO WA YANGA KASEMA NENO HILI TU MOJA… KUHUSU ISHU YA BALEKE KUSEPA CONGO…MANARA AWAPA ZA USO SIMBA….AITAJA GSM…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply