Habari za Yanga
Habari za michezo

WAKATI SIMBA NA AZAM WAKISHUSHA VIFAA VYAO…ENG HERSI KATIKISHA KICHWA KISHA AKASEMA HAYA…

admin July 11, 2023 9:24 pm

Wakati vilabu vya Simba, Azam FC na Singida wakiendelea kutangaza sajili zao kila kunapokucha.

Hali ni tofauti kwa Klabu ya Yanga ambao mpaka sasa wamemtangaza mchezaji mmoja tu kujiunga na Klabu hiyo, tena mzawa Nickson Kibabage kutoka Singida FG.

Mashabiki wa Yanga wanaonekana kuwa na wasiwasi huku ikizingatiwa Klabu hiyo imeachana na nyota wake kadhaa.

Sasa Rais wa Klabu ya Yanga Injinia Hersi Said ametoka hadharani na kuwapa matumaini Wananchi na kuwapa neno la Matumaini.

Akizungumza Hersi amesema;

“Naona watu wanaposti sajili zao na kutamba mitandaoni wanayanga wasitishike kwani wanayoyafanya sisi tulishayafanya na tutayafanya kwasababu tumesajili na tuna imani na usajili tulioufanya;

“Kwa namna tulivyopata mafanikio Yanga kwenye mashindano ya ndani na kimataifa msimu huu tunahitaji jitihada zaidi ili kuvuka hatua hiyo na kufikia huko tunahitaji uwekezaji kwenye usajili,”

WAKATI SIMBA WAKITAMBA NA BEKI WAO MCAMEROON…YANGA WAMESHUSHA CHUMA HIKI CHA KAZI… PAMOJA NA KUSEPA ZAKE BONGO….HIVI NDIVYO YANGA INAVYOZIDIA KUMPAISHA NABI KIMATAIFA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply