Home Habari za michezo USAJILI WA SIMBA, YANGA SIO POA MNYAMA ATANGAZA KUMSAJILI KIUNGO HUYU WA...

USAJILI WA SIMBA, YANGA SIO POA MNYAMA ATANGAZA KUMSAJILI KIUNGO HUYU WA AL HILAL YA SUDAN

Klabu ya Simba rasmi imekamilisha usajili wa aliyekuwa kiungo wa Al Hilal ya Sudan, Fabrice Ngoma kwa mkataba wa miaka miwli kwa ajili ya kuimarisha eneo la kiungo la kikosi hicho kwa msimu mpya wa mashindano 2023/2024.

Usajili wa Ngoma umehitimisha kiu ya miaka minne ambayo Simba imekuwa nayo tangu wamtake 2019 akichezea AS Vita ya DR Congo kisha akatimkia Raja Casablanca ya Morocco.

Simba ilivutiwa na kiwango cha nyota 2019 katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na AS Vita lakini hawakufanikiwa kunasa saini yake walipozidiwa kete na Raja.

Hata hivyo machafuko ya kisiasa yaliyotokea huko Sudan miezi kadhaa iliyopita, yalichangia kumfanya mchezaji huyo na nyota wengine kadhaa kuvunja mikataba yao ya kuichezea timu hiyo iliyotwaa taji la Ligi Kuu nchini humo mara 29.

Usajili wa Ngoma unaonekana kulenga kuzipa pengo la nafasi ya kiungo wa ulinzi ndani ya kikosi cha Simba ambalo limetokana na kuonyeshwa mlango wa kwaheri kwa Erasto Nyoni, Jonas Mkude na Ismail Sawadogo.

Kusajiliwa kwa Ngoma mwenye uwezo pia wa kucheza nafasi ya beki wa kati na kiungo mshambuliaji, kunaonekna kumuongezea machaguo kocha wa Simba, Robertinho Oliveira katika nafasi ya kiungo wa ulinzi ambayo kwa sasa ana wachezaji wawili tu anaowategemea ambao ni Mzamiru Yassin na Sadio Kanoute.

SOMA NA HII  NUNGUNUNGU ALIWA KICHWA JANGWANI...KAMWE AFUNGUKA