Habari za SImba SC
Habari za michezo

WAKATI CHAMA AKIITINGISHA KIBERITI SIMBA…MO DEWJI ALIPUA JAMBO HUKO….

admin July 17, 2023 9:27 pm

Baada ya majadiliano na uongozi kumalizika vizuri, Kiungo Mshambuliaji Clatous Chama ataondoka nchini muda wowote kutoka sasa kuelekea Uturuki kujiunga na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao 2023-24.

Kwa mujibu wa taarifa ambayo Simba wameitoa leo Julai 17, 2023, Chama ataondoka pamoja na kiungo mkabaji Fabrice Ngoma ambaye mchakato wa kupata vibali vya kuingia Uturuki unaendelea vizuri.

Wawili hao wakifika Uturuki itakuwa wachezaji wote waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao watakuwa wamekamilika.

MO DEWJI KAMA KAWAIDA YAKE

Saa chache kabla ya taarifa za kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama kujulikana hatma yake, Rais wa Heshima na Mwekezaji wa klabu hiyo Mohamed Dewji alimuibua mchezaji huyo kimafumbo.

Mo Dewji alitwiti kwenye ukurasa wake wa Twitter maneno ambayo yaliashiria kuna mchezaji anawasumbua lakini Simba ikiamua jambo lake haishindwi.

“Huyu mchezaji mkubwa ambaye ana mkataba na timu kubwa, mbona analeta tabu, Simba ikiamua jambo limeamua,” alitwiti Mo.

Lakini hata hivyo, dakika kadhaa mbele, Simba walitangaza kumalizana na Chama na ataungana na wenzake kambini Uturuki.

ENDELEA KUVUNA MKWANJA KUPITIA MERIDIANBET…. SIMBA ILIVYOMNASA MIQUISSONE KIMAFIA, SINEMA ILICHEZWA KWA SIRI, ASUBURIWA KWA HAMU UTURUKI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply