Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally alisema atakuwa sehemu ya kuongoza msafara wa uzinduzi wa jezi mpya watakazovaa kwa msimu wa 2023/24.
Alisema tamasha la Simba Day limerudishwa nyuma awali lilitakiwa kufanyika Agosti 8, mwaka huu sasa imerudishwa siku moja nyuma kwa sababu ya kuwapa muda wachezaji wao kupumzika.
“Kutokana na taratibu kutokuwa rafiki ya Agosti inatulazimu kucheza Agosti 6 badala 8, ambayo tunatarajia kusafiri kuelekea Tanga kwa sababu tarehe 10 tutakuwa na mechi yetu ya Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fountain Gate.
Tukifanya Agosti 6 na 7 wanatarajia kwenda Tanga na wachezaji kupumzika na kuwapa kujiandaa na mechi yetu hiyo ninaimani tutawafunga tu maana msimu huu hatutaki kuacha kitu,” alisema Ahmed.
Aliongeza kuwa tiketi na mipango yote kuhusu tamasha hilo na utaratibu wa Viingilio wataviweka hadharani katika mitandao yao juu ya nini kitafanyika siku hiyo.
“Usajili unaendelea bado mchezaji mmoja na viongozi wa Simba wasikivu sana, sasa ni zamu ya mmakonde (Luis Miquissone) usajili ambao wanaousubiri sasa wanasimba kuuona kwa sasa.
Kwa sasa Simba kuna mmakonde mmoja (mimi) sasa bado mmakonde mwingine kutua ndani ya kikosi cha Simba, vuta picha kikosi yupo Aubin (Kramo), Willy Essomba Onana, Jean Baleke halafu kuna Miquissone,” alisema Ahmed aliongeza
Safari wapinzani wajiandae maana Simba ni tishio ukiachilia nyota hao kuna Clatous Chama, ambaye kuna watu wanamuota na wataendelea kumtamani tu hawampati”.
Mshambuliaji mpya wa Simba, Onana alisema anawaskuhuru sana uongozi wa Simba, Mashabiki kuhakikisha anawapa furaha kwa kupambani timu kufikia malengo yao.
“Siwezi kuzungumza sana kwa sababu kazi yangu itaonekana uwanjani, nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kufanya kila kitu pamoja na wachezaji wenzangu ili kuwapa furaha mashabiki,” alisema Onana.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Banki ya NMB filbert Mponzi alisema ushirikiano kati ya Simba na banki yao utakuwa na mafanikiwa makubwa kwa mashabiki wa klabu hiyo.
Alisema katika ushirikiano huo utawanufaisha mashabiki na wanasimba kwa kufungua Akaunti ya Simba, Queens (Malkia kwa wanawake), Platinum na Watoto.
“Kadi moja itatumika katika utambulisho wa wanachama wa klabu ya Simba na kufanyia muamala pia wanafaidika kwa kupata bima ya maisha au ulemavu na kupata Mkopo fantastic, pia kutakuwa na Akaunti ya watoto,” alisema Mponzi