Home Uncategorized HATMA YA ZAHERA NA YANGA JUU YA MKATABA MPYA HII HAPA

HATMA YA ZAHERA NA YANGA JUU YA MKATABA MPYA HII HAPA


UONGOZI wa Klabu ya Yanga upo mbioni kumuongezea mkataba mpya kocha wake mkuu Mkongomani, Mwinyi Zahera wa kuendelea kukinoa kikosi hicho. Mkongomani huyo alijiunga na Yanga katikati ya msimu wa mwaka juzi akitokea Builcon FC ya Zambia.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa ni kuwa Yanga ipo kwenye mchakato wa mwisho wa kukamilisha mpango huo wa kumuongezea mkataba mara baada ya kurejea jijini Dar es Salaam akitokea Misri anapofanya majukumu ya timu ya taifa lake la DR Congo katika michuano ya Afcon.

Mtoa taarifa huyo alisema kama mazungumzo yakienda vizuri, basi atasaini mkataba wa miaka miwili ya kuendelea kukinoa kikosi hicho kitakachoundwa na wachezaji zaidi ya 12 wapya waliosajiliwa.

“Hivi sasa uongozi upo kwenye mipango ya kukisuka kikosi chetu kwa kusajili wachezaji wapya huku wengine tukiwaongezea. “Tupo kwenye mazungumzo na kocha wetu Zahera kwa ajili ya kumuongezea mkataba mpya wa kuifundisha Yanga.

“Pia, msaidizi wake Mwandila (Noel) raia wa Zambia ambaye mkataba wake umemalizika baada ya kupokea mapendekezo ya Zahera kuwa anahitaji kuendelea kuwa pamoja na kocha huyo,” alisema Mwakalebela

SOMA NA HII  MAREKANI YASEMA VIRUSI VYA CORONA NI FURSA KWAO