Habari za michezo

MALONE AFUNGUKA KILA KITU KUHUSU YEYE KUTUA SIMBA

Staff Desk July 20, 2023 7:36 pm

MLINZI mpya wa Klabu ya Simba Che Malone Fondoh amesema aliamua kujiunga na timu hiyo ili kuonesha daraja alilo nalo anapokuwa dimbani.

Che Malone amesema anafahamu Simba kuna wachezaji wenye ubora mkubwa hasa katika nafasi anayocheza lakini siku zote amekuwa ni mtu wa kufanya juhudi hivyo hana wasiwasi anaamini atapata nafasi ya kucheza ndani ya kikosi cha miamba hiyo ya mitaa ya Msimbazi Dar es Salaam.

Malone ameongeza kwa kusema timu nyingi zilihitaji huduma yake lakini aliamua kuichagua Simba kutokana na klabu hiyo kuonesha nia ya dhati ya kuitaka huduma yake.

Kauli hizo za Mlinzi huyo wa kimataifa wa Cameroon amezitoa wakati akifanya mahojiano na Runinga ya mtandaoni ya klabu ya Simba.

BAADA YA YANGA KUMCHUKUA MKUDE, SIMBA YAMLETA MBADALA WAKE SLOTI YA WANYAMA KUSHINDA NI RAHISI SANA JARIBU SASA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply