Habari za michezo
KOCHA WA YANGA AIMWAGIA SIFA YANGA, GAMONDI ATAMBA
Staff Desk
July 21, 2023
3:28 pm
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema timu hiyo inatarajia kuwa na malengo makubwa zaidi kwa sababu ni klabu kubwa yenye mashabiki wengi wenye nguvu na ushawishi kutaka iendelee kufanya vizuri zaidi hasa kwenye mashindano ya kimataifa.
Gamondi amesema hayo leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam kuelekea kilele cha tamasha la siku ya Mwananchi kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.
“Kesho ni siku kubwa kwa mashabiki wa Young Africans SC pamoja na sisi wote tunakwenda kupata nafasi ya kusherekea kufunguliwa kwa msimu huu mpya tukiwa na matarajio ya kuendelea kuipambania klabu hii kubwa yenye historia kubwa” amesema Gamondi.
Kocha huyo mpya wa Yanga kutoka Argentina amesema atautumia mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Kaizer Chiefs kesho kama sehemu ya maandalizi ya klabu hiyo kwa msimu ujao.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.