Home Habari za michezo MWENYEKITI WA SIMBA AUAWA NA WATU WASIO JULIKANA

MWENYEKITI WA SIMBA AUAWA NA WATU WASIO JULIKANA

Morogoro. MWENYEKITI wa tawi la Simba SC katika mji mdogo wa Mchombe kata ya Mngeta Halmashauri ya Mlimba, Benson Mwakasanga (48) amefariki dunia baada ya kudaiwa kushambuliwa na kundi la watu wasiojulikana usiku wa kumkia leo Julai 25 akiwa shambani katika mavuno ya zao la mpunga wilaya ya Kilombero mkoani hapa.

Mwakasanga amekutwa amepoteza maisha huku mwili wake ukiwa na majeraha sehemu mbalimbali yanayaodhaniwa kifo chake kimetokana na kujeruhiwa na kitu chenye nchi kali.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Julai 25, 2023, Msemaji wa tawi hilo, Supertus Duma amesema Mwakasanga amekutwa amefariki dunia asubuhi ya leo huku mwili wake ukiwa na majeraha maeneo ya kichwani, kifuani na mikononi hali inayoashiria kuwa kabla ya kifo chake kulikuwa na mapambano.

Duma amesema Mwakasanga licha kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba tawi la Mngeta alikuwa akijishughulisha na shughuli za kilimo na umauti unamkuta alikuwa shamba akivuna zao la mpunga.

“Amekuwa mwanzishi wa tawi la klabu ya Simba SC Mngeta wilaya ya Kilombero na amekuwa Mwenyekiti tangu kuanzishwa Kwake mwaka 2000 na uwepo wa majeraha katika mwili wake ni ishara kuwa kabla ya Mwakasanga alipambana na huenda katika kuzidiwa nguvu ndio iliyopelekea kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake na inaonyesha alipoteza damu nyingi,” amesema Duma

Duma amesema aliongea naye jana saa 4 usiku wa Julai 24 na kupewa mipango ya kuandaa safari ya Simba Day na saa 5 usiku huo pia aliongea na mtoto.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema tukio hilo limeripotiwa kwa jeshi hilo na maafisaa wa jeshi la polisi linakusanya taarifa ili kutoa taarifa kwa umma.

SOMA NA HII  MSEMAJI WA SIMBA AFUNGUKA HAYA BAADA YA KUTAJWA FIFA