Facebook Instagram Linkedin Mail Twitter Website Youtube
  • Home
  • TAIFA STARS
  • SIMBA SC
  • YANGA SC
  • AZAM FC
  • KIMATAIFA
  • BURUDANI
Search
Tuesday, July 15, 2025
  • Blog
  • Forums
Facebook Instagram Linkedin Mail Twitter Website Youtube
Soka La Bongo
  • Home
  • TAIFA STARS
  • SIMBA SC
  • YANGA SC
  • AZAM FC
  • KIMATAIFA
  • BURUDANI
Home Habari za michezo KIPA MBRAZIL WA SIMBA ATAKIWA KUTHIBITISHA UBORA WAKE, KIPA WA MAKOCHA AFUNGUKA...
  • Habari za michezo
  • Habari za Simba
  • Habari za Simba Leo
  • Michezo
  • Michezo Bongo
  • Michezo Soka la Bongo
  • news
  • Simba SC

KIPA MBRAZIL WA SIMBA ATAKIWA KUTHIBITISHA UBORA WAKE, KIPA WA MAKOCHA AFUNGUKA KILA KITU, MANULA ATAJWA

Share
Facebook
Twitter
Pinterest
WhatsApp
    kipa wa simba

    KIPA wa zamani na kocha wa makipa, Ivo Mapunda amesema kipa mpya wa Simba, Jefferson Luis Szerban anatakiwa kuthibitisha ubora wake kwani ameingia kwenye timu ambayo ina kipa namba moja wa timu ya Taifa, Aishi Manula.

    Simba imemsajili kipa huyo raia wa Brazil kwa mkataba wa miaka miwili, kipindi hiki ndiye atakuwa akisimama langoni kwani Manula anauguza majeraha yake na atakuwa nje ya uwanja kwa miezi mitatu.

    Akizungumza na Mwandishi, Ivo ambaye aliwahi kuzidakia Yanga, Simba, Azam FC na Taifa Stars alisema anaamini Manula atakapopona atarudi kwenye ubora wake na ndiye kipa namba moja wa Simba.

    “Wote wana changamoto, ni ngumu sana kupambana na kipa namba moja wa timu ya Taifa, inawezekana ni kipa mzuri ila anapaswa kufanya kazi kubwa kuhakikisha anawapa Simba kile walichokitarajia na kinachozidi ubora wa Manula.

    “Sio kila mchezaji wa kigeni anayesajiliwa anakuwa na uwezo wa kucheza, Luis ametoka kwenye nchi ambayo soka limezaliwa huko, tunapenda kuona tofauti yake kwa kiwango kikubwa,” alisema Ivo.

    Ivo alisitiza anamfahamu Manula hata kama ana mapungufu ambayo hayamfanyi kutokuwa namba moja ndani ya Simba upande wa makipa.

    “Kuuguza majeraha kuna mwisho na ninavyomfahamu Manula hawezi kukubali kupoteza namba kwa sababu tu ametoka kwenye majeraha, ni kipa mpambanaji, namba yake iko wazi kabisa pale Simba. Urefu wa Mbrazili huyo anaweza akawa mzuri mipira ya juu pengine hata ya chini, hii haizuii ila atuonyeshe ubora wake wa kumzidi mzawa.”

    Simba imemsajili kipa huyo kutoka Resende FC ya Brazil na msimu uliopita ameichezea Itabirito FC-MG kwa mkopo na yupo kambini Uturuki.

    Kwa usajili huo Simba inakuwa na makipa wanne Manula, Ally Salim, Ahmed Feruzi ‘Teru’ pamoja na Jefferson.

    SOMA NA HII  BAADA YA YANGA KUANZA KUMFUKUZIA...SIMBA NAO WANOA NDOANO KUMNASA AZIZ KI..MAMBO YAKO HIVI..
    Previous articleWAWAKILISHI WA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA, SIMBA, YANGA, AZAM, SINGIDA FG, RATIBA KAMILI IKO HIVI
    Next articleBANGALA AFUNGUKA MAZITO KABLA YA KUSEPA, HUYO MRITHI WA MAYELE ANAMTIHANI HUU HAPO YANGA
    Staff Desk

    RELATED ARTICLESMORE FROM AUTHOR

    Habari za Yanga leo
    Habari za michezo

    SIKU YA KOCHA MPYA YANGA YATANGAZWA….CV YAKE BABU KUBWA HAKUNA TZ….

    Habari za Simba leo
    Habari za michezo

    MASHINE HII YA KAZI KUTUA KUMSAIDIA ‘TSHABALALA’ SIMBA…. BEKI NA GOLIKIPA MPYA NDANI…

    Habari za Simba leo
    Habari za michezo

    HIZI HAPA MASHINE 9 ZA KAZI KUTUA SIMBA….FADLU ATIA UBANI…FEI TOTO NDANI…..

    Sign in
    Welcome! Log into your account
    Forgot your password? Get help
    Password recovery
    Recover your password
    A password will be e-mailed to you.

    LEAVE A REPLY

    Log in to leave a comment

    329,001FansLike
    12,344FollowersFollow
    16,900SubscribersSubscribe
    FcTables.com

    EDITOR PICKS

    PASIPOTI YAMZUIA AIYEE KWENDA SWEDEN

    admin - June 17, 2019

    CAF WASEMA WAKUBWA NI HAWA…….. DABI INAFIA HAPA

    Staff Desk - November 2, 2023

    KUELEKEA KARIAKOO DABI….CHAMA, PHIRI NA BOCCO WATOLEWA CHAMBO…AHMED ALLY AANIKA SABABU…

    admin - October 21, 2022

    PAMOJA NA KUTAMBULISHWA KWA MBWEMBWE…GAMONDI AMPIGA STOP OKRAH…

    admin - February 1, 2024

    CleverntAD
    Facebook Instagram Linkedin Mail Twitter Website Youtube
    • Disclaimer
    • Privacy
    • Advertisement
    • Contact Us
    © Soka la Bongo Online Media | Designed by Yatosha Web