hafiz konkani
Habari za michezo

HUYU HAPA MRITHI WA MAYELE, ATAMBULISHWA USIKU MNENE

Staff Desk July 30, 2023 10:37 am

Klabu ya Yanga imefanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji, Hafiz Konkoni (23) Bechem United ya Ghana kwa kandarasi ya miaka miwili.

Konkoni ambaye amesajiliwa kuziba pengo la Mkongomani Fiston Mayele anayetajwa kujiunga na Pyramid ya Misri baada ya msimu uliopita kumaliza na mafanikio ya kuwa mfungaji bora Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika.

Mrithi huyo wa Mayele msimu uliopita katika ligi ya Ghana alifanikiwa kufunga mabao 15 kwenye mechi 26 na kutoa assist 3 akimaliza nafasi ya pili.

Kabla ya Konkoni kusajiliwa na Yanga alikuwa akihusishwa klabu ya Al Hilal ya Sudan.

LIGI KUU BARA 2023/24 MACHO YOTE KWA MAKOCHA, YANGA NA KOCHA WAO MPYA SASA DILI LA MAHOP LAINGIA MDUDU, HUKU CAF IKITOA SIKU TATU TU KWA YANGA, ISHU IKO HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply