Steve Barker Simba Day
Simba SC

Kocha Steve Barker Aweka Wazi Mipango ya Simba Day Dhidi ya Police FC

Vardo August 7, 2026 5:30 pm

Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, amesema mchezo wa kirafiki dhidi ya Police FC kutoka Kenya utakaochezwa kesho katika kilele cha Simba Day utakuwa kipimo muhimu na cha mwisho kwa kikosi chake kuelekea msimu mpya wa 2026/27.

Barker ameeleza kuwa maandalizi ya timu hiyo yamekwenda vizuri na wiki hii imekuwa ya mafanikio makubwa katika kujenga kikosi imara kitakachokuwa na ushindani wa hali ya juu.

Kuelekea mchezo huo wa kesho, kocha huyo alisema kuwa Simba Day ni zaidi ya tamasha la kuwakutanisha mashabiki na timu yao. Ni fursa ya pekee kwa benchi la ufundi kutathmini kiwango cha wachezaji kwenye mazingira halisi ya ushindani.

“Biashara kamili itaanza wiki ijayo. Tunahitaji kutumia mchezo wa kesho kupata picha halisi ya kiwango tulichofikia kabla ya kuanza rasmi kwa ligi,” amesema Barker.

Aliongeza kuwa mashabiki watapata nafasi ya kuona sura mpya za wachezaji waliosajiliwa pamoja na muunganiko wa kikosi kizima kabla ya kuanza rasmi kwa mechi za ushindani.

Duchu Aahidi Burudani kwa Mashabiki

Kwa upande wake, kiungo wa Simba, David Kameta ‘Duchu’, amesema maandalizi yao yamekamilika na wako tayari kutoa burudani.

Duchu ameeleza kuwa mchezo huo dhidi ya Police FC utakuwa fursa nzuri kwao kuonyesha yale yote waliyoyafanyia kazi mazoezini na kuahidi kuwa mashabiki watashuhudia kiwango safi kutoka kwa kila mchezaji.

Tamasha la Simba Day linatarajiwa kuwa jukwaa kuu la kuwatambulisha wachezaji wote wapya na wa zamani watakaoipigania Simba SC katika msimu wa 2026/27.

Meridianbet Yawapa Wachezaji Bahati ya Kwanza Kupitia 3 Fisher Cats Neo Maema Arejea Simba SC: Azua Gumzo Mazoezini Kuelekea Simba Day 2026