Neo Maema Simba SC
Simba SC

Neo Maema Arejea Simba SC: Azua Gumzo Mazoezini Kuelekea Simba Day 2026

Vardo August 7, 2026 5:35 pm

KIUNGO mshambuliaji raia wa Afrika Kusini, Neo Maema, ameonekana kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Simba SC tangu kumalizika kwa msimu uliopita, akitoa ishara ya wazi ya kuanza ukurasa mpya katika maandalizi ya msimu wa 2026/27.

Maema, ambaye mkataba wake wa awali wa mkopo kutoka Mamelodi Sundowns ulikuwa umemalizika, amerejea klabuni hapo baada ya viongozi wa pande zote mbili kufikia makubaliano ya pamoja pamoja na mchezaji mwenyewe.

Uongozi wa Simba SC umefanya jitihada kubwa kuhakikisha kiungo huyo fundi anasalia Msimbazi kwa kuingia mazungumzo mapya na mabosi wa Mamelodi Sundowns, ambapo taarifa za ndani zinaeleza kuwa wamefanikiwa kumuongeza kwa mkataba mwingine wa mkopo wa msimu mmoja zaidi.

Asubuhi ya leo, Maema ameonekana akishiriki kikamilifu mazoezi ya mwisho ya Wekundu wa Msimbazi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Uwepo wake mazoezini unaashiria kuwa ni sehemu muhimu ya mipango ya benchi la ufundi kuelekea msimu mpya wa mashindano.

Mashabiki wa Simba wanatarajia kumuona Maema akitambulishwa rasmi kesho, Jumamosi, Agosti 8, 2026, katika tamasha kubwa la kilele cha Simba Day litakolofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kocha Steve Barker Aweka Wazi Mipango ya Simba Day Dhidi ya Police FC Mo Dewji Awataja Kocha na Wachezaji Bora Wa Muda Wote Simba SC