Home Habari za michezo KLABU YA SINGIDA FOUNTAIN GATE IMEELEZA MALENGO YAKE, HUKU AKILI YOTE IPO...

KLABU YA SINGIDA FOUNTAIN GATE IMEELEZA MALENGO YAKE, HUKU AKILI YOTE IPO KWA SIMBA

CEO Mpya Singida Fountain Gate FC

Klabu ya Singida Fountain Gate, imeweka wazi malengo yao kuelekea msimu ujao wa michuano yote watakayoshiriki msimu wa 2023/24, huku ikishindwa kukunjua makucha yao katika suala zima la kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Вага.

Singida Fountain Gate FC, katika msimu wa 2022/23, ilifanya vizuri kwa kumaliza nafasi ya tatu katika Ligi Kuu hivyo kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu ujao.

Afisa Habari wa Singida Fountain Gate FC, Hassan Masanza, amesema malengo yao ya awali ni kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika kila mashindano wanayoshiriki ikiwamo kumaliza nafasi tatu za juu kwenye ligi.

Amesema kwenye mashindano mingine ikiwamo Ngao ya Jamii, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’, Kombe la Mapinduzi linalofanyika kila mwaka visiwani Zanzibar, wanahitaji kufika Fainali na michuano ya kimataifa kutinga hatua ya makundi.

“Malengo yetu ya chini ambayo klabu yetu imeyaweka kwa msimu wa 2023/24, matarajio yetu tutafikia malengo hayo kwa asilimia 100 kama tulivyofikia msimu wa 2022/23.

“Matumaini yetu makubwa ni kufikia malengo hayo na ninaimani tutafika kwa kuwa tumefanya usajili mzuri kulingana na mahitaji ya timu kwa kufuata mapendekezo ya benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Hans van Pluijm,” amesema Massanza.

Wakati bado mchakato wa kuimarisha kikosi cha timu hiyo ukiendelea, timu hiyo imeingia kambini leo jijini Arusha kikiwa huko kitapata michezo miwili ya kirafiki na timu mbili kutoka nje ya Tanzania, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao, na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba SC.

Hadi sasa Singida Fountain Gate FC imetangaza usajili mpya ambao ni Yahya Mbegu kutoka Ihefu FC na beki wa Simba SC, Joash Onyango aliyejiunga na timu hiyo kwa mkopo wa msimu mmoja.

SOMA NA HII  KISA USAJILI WA AZIZ KI NA KAMBOLE...NABI ASHINDWA KUJIZUIA YANGA...ADAI KUNA MTU ANAMTAFUTA..."SITAKI KUYUMBA"...