Home Habari za michezo WAKATI SHABAN DJUMA AKIENDELEA KUZILA ….CHUMA HIKI HAPA KINATUA TZ KUMRITHI PALE...

WAKATI SHABAN DJUMA AKIENDELEA KUZILA ….CHUMA HIKI HAPA KINATUA TZ KUMRITHI PALE YANGA…

Tetesi za usajili Yanga

Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans leo Jumanne (Julai 11) ulitarajiwa kumpokea beki wa kulia wa ASEC Mimosas ya vory Coast, Kouassi Atohoula, kwa ajilí ya kukamilisha shughuli ya Kusaini mkataba, kisha kutambulishwa rasmi kama mrithi wa Djuma Shaban.

Chanzo kutoka Young Africans kimeeleza kuwa, tayari nyota huyo ameshakamilisha kila kitu kwa ajili ya kutua klabuni hapo, na alitarajiwa kutua jana Jumatatu (Julai 10).

Tunamshukuru Mungu baada ya Djuma Shaban kuonesha hali ya kugomea mkataba mpya na kupishana kauli kwenye mambo kadhaa na uongozi, mara moja tuaanza taratibu za kutafuta mbadala wake ambapo tayari tumekamilisha usajii wa beki wa kulia kutoka ASEC Mimosas ya lvory Coast, Kouassi Attohoula na atatua nchini juma hili tayari kwa kuinga kambini na wenzake, kimesema chanzo hicho.

Afisa Habari wa Young Africans, Ally Kamwe amesema: “Leo wachezaji wote wataanza kuingia nchini kwa ajii ya kambi ya maandalizi ya msimu ujao, wataungana na wachezaji wapya wote ambao usajili wao umekamilika, kisha tutaanza kutangaza mmoja baada ya mwingine.”

SOMA NA HII  LWANDAMINA 'APIGA MKWARA WA KUFA MTU' YANGA.....AJITABIRIA MAKUBWA...