Habari za michezo

HUKO SIMBA DAY FULL SHANGWE SAMIA MGENI RASMI

Staff Desk August 4, 2023 10:50 am

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha ya Simba Day litakalofayika keshokutwa Jumapili (Agosti 06), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Simba SC imethibitisha taarifa za Rais Samia kutarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Simba Day, kupitia vyanzo vya habari vya klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi jijini Dar es salaam.

Siku hiyo Wachezaji waliosajiliwa Simba SC kwa msimu 2023/24 watatambulishwa rasmi kwa Mashabiki na Wanachama, huku wakitarajiwa kucheza mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Mabingwa wa Soka nchini Zambia Power Dynamos.

Mbali na matukio hayo mawili, pia kutakuwa na shamra shamra nyingi za burudani kutoka kwa wasanii wa muziki.

Taarifa iliyothibitisha hilo imeandikwa: Karibu kwenye kilele cha Wiki ya Simba. Karibu kwenye Simba Day, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hii ni siku muhimu kwa Klabu ya Simba na wapenda michezo wote nchini Tanzania.

Tunakushukuru na tanakukaribisha kwa furaha kubwa isiyo na kifani. Kwa kipekee kabisa, tunakushukuru sana kwa mchango wako mkubwa kwenye sekta ya Michezo na Maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Karibu sana Mheshimiwa Rais.

SIO SIMBA,YANGA WALA AZAM HAWACHEKANI TENA MAANA MABO YENYEWE YAPO HIVI GAMONDI AFUNGA PRE-SEASON YANGA KIBABE….. JUMATATU TANGA HAPAKALIKI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply