Home Habari za michezo HUO UTAMBULISHO WA SIMBA DAY SIO POA

HUO UTAMBULISHO WA SIMBA DAY SIO POA

Utambulisho wa wachezaji ulianza saa 10: 36 kubwa ni zawadi ambayo ikutarajiwa na mashabiki utambulisho wa kipa mpya mzawa kutoka KMC FC, Hussein Abel ambaye anaungana na makipa wengine wa klabu hiyo akiwemo Ahmed Feruz, Ally Salim na Aishi Manula.

Mabeki Shomari Kapombe, David Kameta, Jimmyson Mwanuke, Mohamed Hussein, Israel Patrick, Kennedy Juma, Hussein Kazi, Che Fondoh Malone na Henock Inonga Bacca.

Viungo ni Abdallah Hamis, Mzamiru Yasin, Sadio Kanoute, Nassoro Kapama, Fabrice Ngoma, Clatous Chama, Willy Essomba Onana, Aubin Kramo, Peter Banda, Saido Ntibazonkiza, Kibu Denis, Shaban Chilunda, John Bocco, Mohamed Musa, Jean Balek, Moses Phiri na Luis Miquissone.

Jumla ya wachezaji 30 wametambulishwa ambao wataitumikia Simba kwa msimu mpya wa 2023/24 na benchi la ufundi likiendelea kuwa chini ya Roberto Oliveira Robertinho.

Hili ni tamasha la 15 kufanywa na Simba tangu lilipoasisiwa na aliyekuwa mwenyekiti wao Mzee Hassan Dalali pamoja na Katibu Mkuu mkuu wake Mwina Kaduguda,Nahodha msaidizi Mohammed Hussein, mchezaji mwandamizi zaidi kwenye kikosi cha Simba hivi sasa akiwa amedumu kwa misimu tisa tangu aliposajiliwa mwaka 2014 akitokea Kagera Sugar, ikiwa Simba Day yake ya 10.

MASHABIKI KUINGIA UWANJANI:

Tamasha la Simba Day mwaka huu limeweka rekodi ya kujaza uwanja zikiwa zimebaki siku tatu kabla ya mchezo Mageti yalifunguliwa saa 2:00 asubuhi ili kupunguza msongamano wa watu kuingia na kufika saa 4:30 asubuhi tayari upande wa viti vya mzunguko vilikuwa vimeanza kujaa.

Hadi saa 6:00 mchana jukwaa la  viti vya Orange mashabiki waliingia na kujaza nafasi hiyo, kufika saa 7:30 mchana uwanja ulikuwa umejaa.

MCHEZO WA KIRAFIKI TIMU YA WANAWAKE NA VIJANA:

Timu ya Simba Queens imecheza mechi ya kirafiki dhidi ya Masala Princess, Malkia wa Wekundu wa Msimbazi hao kuibuka na ushindi wa mabao 4-0, yakifungwa na Asha Djafari (2), Joelle Bukuru (1) na Shelda Boniface (1)

Mechi nyingine ya timu  ya Simba vijana kwa kucheza wenyewe kwa wenyewe huku timu ya kwanza ikipewa jina la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na timu nyingine ikipewa jina la Makamu wa Rais Dk Phillip  Mpango.

Timu ya Rais Dk Samia ikiwa imevalia jezi za  rangi nyeupe ambayo Kocha wake alikuwa Selemani Matola na ya Makamu Mpango ilivaa uzi wa rangi nyekundu. Kikosi kilichopewa Samia Boys kimeshinda mabao 3-1 dhidi ya Mpango Boys.

BURUDANI KUANZA:

Saa 5:35 asubuhi Burudani ya Muziki ilianza baada ya wasanii mbalimbali kupanda katika jukwaa maalum kwa ajili ya kuburudisha mashabiki elfu 60,000 waliopo uwanjani.

Saa 6:17 mchana  Bendi ya Twanga Pepeta inayomilikiwa na Mjumbe wa Bodi ya Simba, Asha Baraka ilitoa burudani kwa kuimba nyimbo ya ‘Angurumapo Simba’ ambayo ilikuwa kivutio cha mashabiki ndani ya uwanja wa Benjamin Mkapa.

Wasanii mbalimbali wakitoa burudani akiwemo John Simon ‘Joh Makini’ na Meja Kunta,  Tunda Man ametia fola kwenye tamasha hilo kwa kuingia kwa staili ya mfungwa na kibao chao cha ‘Simba sihami’.

Kikundi cha Sarakasi cha jijini Mwanza kilipanda Jukwaani saa 9:18 na kutoa burudani.

,Ally  Saleh ‘Ali Kiba’, ni msanii wa mwisho katika orodha ya watu waliotoa burudani ambapo alipanda jukwaa saa 9:37 na kukata  kiu ya mashabiki waliojitokeza kwa wingi kushuhudia kikosi kipya cha Wekundu hao wa Msimbazi wa msimu huu unaotarajiwa kuanza Agosti 9, mwaka huu kwa mechi za Ngao ya Jamii.

KITUKO CHA MENEJA WA IDARA YA HABARI NA MAWASILIANO:

Saa 10 :00 alasiri Ahmed Ally amefanya kituo cha mwaka kwa kuingia uwanjani na Ngamia kwa ajili ya kutambulisha wachezaji na benchi la ufundi.

Wakati huo huo Rais wa heshima na Muwekezaji wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji aliingia uwanjani saa 10: 21 ambapo mashabiki walifurahi kwa kumuona Billionea huyo.

@@@@

SOMA NA HII  KISA SIMBA...YANGA KULIPA MAMILIONI YA PESA FIFA....BARUA YATUA KWA MABOSI TFF....