Hans Van De Pluijm kocha wa Singida Big Stars atamani kuifundisha Simba
Habari za michezo

KOCHA WA SINGIDA FOUNTAIN GATE AITAMBIA SIMBA, KAZI IPO HUKO TANGA

Staff Desk August 6, 2023 1:41 pm

Kocha Mkuu wa Singida Fountain Gate, Hans Van Pluijm amesema ameridhishwa na kiwango cha wachezaji wake na sasa wapo tayari kuikabili Simba SC kwenye mchezo wao wa Ngao ya Jamii utakaofanyika Alhamis (Agosti 10) kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga.

Pluijm amesema kiwango walichokionyesha wachezaji wake kwenye mchezo wao kimataifa wa kirafiki dhidi ya AS Vita uliochezwa Jumatano(Agosti 02) kimemfurahisha na kumemuaminisha kuwa sasa wapo tayari kwa ligi kuu na michezo yote iliyopo mbele yao.

Kocha huyo kutoka Uholanzi amesema wachezaji wake walicheza mechi hiyo kwa bidii na kujituma, hivyo ana uhakika kama wataendelea kucheza hivyo kwenye mechi zinazofuata hana shaka na ushindi kwani anaviamini viwango vya wachezaji wake.

SIMBA DAY YAWANG’ARISHA MASTAA HAWA HUKO SIMBA UNYAMA UNYAMA, HISTORIA MPYA IMEANDIKWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply