Home Habari za michezo MASTAA YANGA WAMVURUGA GAMONDI ISHU IKO HIVI

MASTAA YANGA WAMVURUGA GAMONDI ISHU IKO HIVI

Habari za Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ana kazi kubwa ya kufanya kutokana na vita kali iliyopo kwenye eneo la kiungo mshambuliaji kati ya Stephane Aziz Ki na Zouzoua Pacome ambao wote kwa pamoja wametupia katika mechi mbili za kirafiki walizocheza.

Yanga wamecheza mechi mbili za kirafiki na kutupia mabao 16 huku wakiruhusu nyavu zao kutikishwa mara moja tu.

Yanga walianza kucheza dhidi ya Magereza ambapo waliibuka na ushindi wa mabao 10-0 yakifungwa na Keneddy Musonda, Clement Mzize waliofunga matatu-matatu, Pacome, Skudu, Azizi Ki na Max walifunga bao mojamoja.

Juzi kikosi hicho kilimenyana na Friends Rangers na kuibuka na ushindi wa mabao 6-1 huku viungo hao washambuliaji wakitupia bao moja moja.

Azizi Ki ambaye ni msimu wake wa pili ndani ya Yanga alitupia, Pacome pia hakuwa mbali, Mzize, Hafiz Konkoni wote walitupia bao moja moja huku Mzize akitupia kambani mara mbili.

Ujio wa Pacome umeibua vita mpya katika eneo hilo la kiungo mashambuliaji kwani masimu uliopita kulikuwa na mzawa Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye ametimkia Azam FC na sasa ni Aziz KI na Pacome.

Eneo hilo ambalo ni maalum kwaajili ya kuzalisha mabao kwa kutengeneza nafasi na kufunga msimu ujao litakuwa chini ya viungo hao waliopokezana tuzo ya MVP katika Ligi Kuu ya Ivory Coast kwani msimu wa 2021-22, tuzo hiyo ilibebwa na Aziz Ki na ya msimu uliopita wa 2022-23 ikachukuliwa na Pacome. Patamu hapo!

KONKONI AANZA KUTUPIA

Yanga imemsajili Konkoni kurithi nafasi ya Fiston Mayele ambaye ametimkia Pyramids FC baada ya kuitumikia Yanga kwa misimu miwili.

Konkoni tayari ameanza kutupia hii ni baada ya kufunga bao moja kwenye ushindi wa mabao sita waliyoyapata Yanga dhidi ya Friends Rangers.

Mshambuliaji huyo ambaye anatazamwa na wadau wengi wa soka kama ataweza kuvaa viatu vya Mcongo Mayele kufunga kwake kunaendelea kumpa nguvu ya ushindani ndani ya timu.

Baada ya mchezo huo Yanga jioni ya jana ilicheza tena na JKU, Jumatatu inaelekea Tanga kwaajili ya mechi za Ngao ya Jamii.

SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKIMRUDISHA KISINDA BONGO...CHAMA KAWATAZAMA WEE...KISHA KWA 'ZARAU' AKAWAAMBIA HAYA...