Home Habari za michezo RAISI SAMIA AWAKOSHA WADAU WA MICHEZO SIMBA DAY, AFUNGUKA KUHUSU GOLI LA...

RAISI SAMIA AWAKOSHA WADAU WA MICHEZO SIMBA DAY, AFUNGUKA KUHUSU GOLI LA MAMA, KUJUSU UJENZI WA VIWANJA ISHU IKO HIVI

MGENI RASMI wa tamasha la Simba Day Rais Dk Samia Suluhu Hassan amesema ahadi yake iko pale pale ya  kununua kila  bao kwenye timu ambazo itashinda katika mashindano ya kimataifa.

Alisema anatambua kuna timu nne ambazo zinashiriki michuano hiyo ikiwemo Simba na Yanga Ligi ya Mabingwa Afrika na kombe la Shirikisho Afrika zikiwakilishwa na Azam FC pamoja na Singida Fountain Gate FC

“Nawaomba kwenye mashindano yajayo ya CAF tunapaswa kuwa na umoja tuache uhasimu  na ahadi yangu ya kununua bao iko pale pale.

Nazipongeza timu zote zilizofanya vizuri ikiwamo timu ya wasichana chini ya miaka 18 kushinda kombe la CECAFA,” alisema Rais Dk Samia na aliongeza kuwa:

Nawashukuru kwa kunialika ninefurahia mualiko huu hamjaniboa mmejaa kwa wingi nafarijika kuwa sehemu ya tamasha hili ambalo limetuunganisha wazee vijana wanawake kwa wanaume,” alisema Rais Dk Samia.

Alisema kwa dhati anawapongeza Simba kwa makubwa waliyoyafanya kwa kuchangia misaada mbalimbali kwa watoto yatima , wazee na wodi za wakina mama na watoto katika Hospital ya Taifa Muhimbili.

Rais Dk Samia alisema pia kutangaza  utalii wa Tanzania kwa kupeleka kibegi kwenye mlima kilimanjaro kimeitangaza sana Tanzania ni ubunifu mzuri.

“Sote tumeshuhudia rekodi mlizoweka Caf mwaka 1984 mlifika fainali ya kombe la Caf na mwaka 1993 mlipofika fainali za Caf msichoke kuitetea Tanzania.

Serikali ina mpango wa  kujenga viwanja viwili kwenye mikoa ya Arusha na Dodoma vyenye uwezo wa kuchukua watazamaji elfu 30000 ikiwa ni maandalizi ya kuandaa fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2027,” alisema Rais Dk Samia.

Rais Dkt, Samia aliwasiri Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11:28 jioni  na kulakiwa na mashabiki elfu 60, 000 waliojitokeza kwenye tamasha hilo na kwenda moja kwa kwenye sehemu ya kuchezea mpira kwa ajili ya kusalia wachezaji wa timu zote mbili Power Dynamos.

Baada ya kusalimiana na timu zote mbili, Rais Dkt Samia alipiga picha na kikosi cha Simba, Waamuzi wa mchezo huo, timu ya Power Dynamos na viongozi wa klabu ya Simba baadae alitembea kwa ajili ya kusalimia mashabiki wa Simba waliokaa jukwaa la VIP B pamoja na kusaini jezi ya Simba.

Viongizi wengine walikuwepo kushuhudia tamasha hilo ni Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo,  Balozi Dkt Pindi Chana, Naibu Spika wa Bunge la Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu.

Wakati huo huo Mohammed Dewji alisema  kwa heshima na taadhima nakushukuru kukukaribisha katika kilele cha Simba day ikiwa timu hiyo inatimiza miaka 87 tangu kuzaliwa.

“Umefanya makubwa kwa kuvutia watalii na wawekezaji na sisi Simba tutakuunga mkono tutakapocheza michuano ya Ligi ya mabingwa tutavaa Visit Tanzania.

“Umefanya makubwa kwenye michezo na sisi tutakuunga mkono tutaleta mafanikio makubwa kwani katika miaka sita tumecheza robo fainali nne za mashindano ya CAF, kwa sasa ndoto zangu siku moja Simba kushika namba moja Afrika.

Tumefurahishwa na uwepo wako katika tamasha letu, tunatambua mafanikio yako na Simba tunaendelea kuvaa Visit Tanzania kwa kukuunga mkono katika kutangaza Utalii wa Tanzania,

Tunaahidi kuimarisha na kuendeleza soka la Tanzania, tunajitahidi kuleta mafanikio ,” alisema Dewji.

@@@@@

SOMA NA HII  YANGA V SIMBA KWA MKAPA SEPTEMBA 25