Habari za michezo

WAKILI WA YANGA, AWAPIGA DONGO HILI SIMBA SC, MANGUNGU AHUSISHWA

Staff Desk August 9, 2023 11:07 am

Jumapili iliyopita Simba walikuwa na Tamasha lao la “Simba Day” katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Kilele cha Tamasha hilo kilifana sana huku Simba wakipongezwa na wadau mbalimbali wa soak kwa namna walivyofanikisha Tamasha hilo.

Mgeni Rasmi katika Tamsha hilo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Miongoni wa watu waliotoa pongezi zao ni Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga wakili Simon Patrick ambae kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alinogesha sherehe yenu watani hongereni, ila siku nyingine rekebisheni protocol, Mwenyekiti wa Klabu Mzee Mangungu sio wa kukaa VIP A, alipashwa akae hapo na mgeni rasmi kwani yeye ndio Kiongozi wa juu kwenye Klabu.

Je unakubaliana na kauli na ushauri huo wa Wakili Simon Patrick? Tupe maoni yako

MANENO KIDOGOOO…. TUKUTANE SAITI, MBRAZILI : SASA MTAIELEWA SIMBA FEI TOTO LEO NDIO LEO ASEMA HAYA KUITIFUA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply