Habari za michezo

SIMBA KUMSAJILI KIPA HUYU KUTOKA KWA NABI

Staff Desk August 11, 2023 10:56 am

Simba imefikia makubaliano ya kuinasa saini ya kipa, Ayoub Lakred (28) aliyekuwa akiichezea timu ya FAR Rabat ya Morocco inayofundishwa na kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi.

Chanzo makini kutoka ndani ya timu hiyo kimesema makubaliano hayo yamefikiwa ikiwa ni siku chache tangu kuachana na Mbrazili, Jefferson Luis aliyeondolewa kambini nchini Uturuki kutokana na majeraha ya misuli..

“Ni kweli yupo nchini na maongezi hadi sasa yanaendelea vizuri, ni matumaini yetu atakuwa msaada mkubwa kutokana na ushiriki wetu wa mashindano mengi ya ndani na kimataifa,” kilisema chanzo changu.

Usajili wa Lakred unakuwa ni wa pili kwa kipa ndani ya kikosi hicho. Lakred aliyezaliwa Juni 1995, alichezea FAR Rabat, timu nyingine aliyowahi kuichezea ni RS Berkane.

MWISHO WA UBISHI,… MAXI , SKUDU KUOGA MINOTI GAMONDI AKIPIGA MKWARA TRY AGAIN AFUNGUKA KILA KITU KUHUSU SIMBA KWENYE SUPER LEAGUE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply