Clement Mzize Atoa Onyo Zito Ligi Kuu: “Wasubiri Kuona Mara Mbili Yake”
MSHAMBULIAJI nyota wa Yanga, Clement Mzize, ametoa onyo zito kwa mabeki wa Ligi Kuu baada ya kuahidi kurejea kwa kasi mpya msimu huu, akisisitiza kuwa mambo mazuri zaidi yanakuja na kile alichokionesha msimu uliopita kilikuwa ni mwanzo tu.
Mzize, ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha yaliyomsumbua msimu uliopita, ameweka wazi kuwa sasa yupo fiti na anaingia uwanjani akiwa na kiu ya kufanya makubwa zaidi ili kuipigania nembo ya Yanga SC.
Kuzungumza na Kocha Manqoba Mngqithi
Mshambuliaji huyo aliyerejea kikosini amefichua kuwa tayari amefanya kikao na Kocha Mkuu wa Yanga, Manqoba Mngqithi, ili kuweka sawa mipango ya kiufundi na matarajio ya timu kwa msimu huu.
“Malengo yangu ni kufanya vizuri zaidi ya nilivyofanya awali. Pale alipoishia Mzize, mashabiki wasubiri kuona mara mbili yake zaidi,” alisema Mzize kwa kujiamini.
Aliongeza kuwa mazungumzo hayo na benchi la ufundi yammompa picha lillilo wazi kuhusu kile kinachotakiwa kutoka kwake, jambo lililomjengea kujiamini na hamasa kubwa ya kutoa mchango mkubwa uwanjani.
Toleo Jipya la Clement Mzize
Mashabiki wa Yanga sasa wanaweza kutarajia toleo jipya la Mzize ambaye analenga kutumia kila nafasi atakayopata kuthibitisha ubora wake na kuisaidia timu hiyo kutetea na kuwania mataji mbalimbali msimu huu.
Kurejea kwa Mzize kunaongeza ushindani na kina cha kikosi katika safu ya ushambuliaji ya Wananchi, jambo linalotoa wigo mpana kwa kocha katika kupanga kikosi cha ushindi.