Home Habari za michezo KULEKEA MECHI YA KESHO….MBRAZILI SIMBA KAONA ISIWE TABU…KAJA NA HILI JIPYA KWA...

KULEKEA MECHI YA KESHO….MBRAZILI SIMBA KAONA ISIWE TABU…KAJA NA HILI JIPYA KWA YANGA..

Habari za Simba SC

NI Mechi ya kisasi na kutaka kuanza mwanzo mpya wa Msimu wa 2023/24 . Hivi ndio unavyoweza kuizungumzia mechi ya fainali ya ngao ya jamii kati ya Mabingwa Watetezi wa kombe hilo Yanga dhidi ya Simba.

Mchezo huo utakaopigwa saa 1:00 usiku katika uwanja wa Mkwakwani, Tanga ambapo Simba waliingia fainali baada ya kumfunga Singida Fountain Gate FC kwa mikwaju ya penalti.

Yanga nao wametimga hatua hiyo baada ya kumfunga Azam FC kwa mabao 2-0, mchezo uliopigwa katika dimba hilo la Mkwakwani.

Kuelekea mechi ya kesho Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliviera (Robertinho) alisema mchezo wa ‘Derby ‘ ni ‘Derby’, ni muhimu kwa mpira wa Tanzania, mashabiki, viongozi na wachezaji wajibu wao kucheza vizuri.

Alisema kuhusu timu yake ina makundi mawili moja wapo tayari kwa mchezo husika, maisha yake ya mpira anapenda sana kucheza mechi hizo na anajua aina gani ya kucheza katika Derby hiyo.

“Kila mchezaji anajua majukumu yake ikiwemo safu ya ushambuliaji na kutowapa presha kwa sababu anajua umuhimu wa mchezo huo na kazi yangu wachezaji kuonyesha ushindani mkubwa.

Kwangu siangalii benchi la Yanga kuwa ni jipya ninachokifanya ni jinsi ambavyo nimejipanga na wachezaji wangu , “ alisema Robertinho

Kwa niaba ya wachezaji wa Simba, Israel Mwenda alisema maandalizi yamefanyia vizuri juzi, wako tayari kwa mchezo muhimu kwao, mashabiki pamoja na klabu pia.

“Tumejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo wetu wa fainali malengo yetu ni kuanza vizuri msimu kwa kutwaa ubingwa na kuondoa na Ngao ya Jamii,” alisema Mwenda.

Kocha wa Yanga, Miguel Angel Gamondi alisema mechi itakuwa ya ushindani na itakuwa tofauti na mechi zingine kwa sababu ya Derby ambayo inaangaliwa na nchi nzima.

“Najua ni Derby na sio vita, ukiwa kwenye mpira ni junsi tunavyocheza na wachezaji hakuna presha kucheza kwa sababu nimewahi kucheza mechi kubwa kama hizi huko nilipotoka.

Nimefurahi sana kucheza huu mchezo, najua Simba na Yanga ni timu kubwa na inafatiliwa sana ninaimani kesho (leo) katika mchezo huu kuna watu watafurahi na wako watakaolia,” alisema Gamondi.

Dickson Job alizungumza kwa niaba ya wachezaji wa Yanga alisema wako tayari kwa ajili ya mchezo huo kwa sababu wanaitaka hiyo mechi kwa ajili ya kutetea taji lao.

“Wachezaji wote tuko tayari na tunaitaka hiyo mechi, tumefanya maandalizi mazuri na tunasubiri muda ufike ili tukawape furaha mashabiki wetu,” alisema Job.

SOMA NA HII  TAKWIMU ZINAONGEA.....MPAKA SASA CHAMA HOI KWA FEI TOTO...KAACHWA MBALI SANA...