Home Habari za michezo VITA YA NAMBA HUKO YANGA SASA IMESHAKUWA MAJANGA…… WAZAWA WAGOMA

VITA YA NAMBA HUKO YANGA SASA IMESHAKUWA MAJANGA…… WAZAWA WAGOMA

habari za yanga

Kuna vita kubwa ya namba ya namba inayoendelea kambini Yanga ni baada ya wachezaji wazawa kugoma kukaa benchi.

Yanga wapo kambini hivi sasa wakijiandaa na mchezo wa Ngai ya Jamii hatua ya fainali watakaocheza dhidi ya Simba SC Jumapili hii saa moja usiku.

Katika mchezo huo Yanga itawachezesha wachezaji wake wapya ambao imewasajili akiwemo Maxi Zangeli, Pacome Zouzoua, Attohoula Yao na Skudu Makudubele.

Meneja wa timu ya Yanga Walter Harrison alisema kuwa upo ushindani mkubwa wa namba hivi sasa katika kikosi hicho kati ya wachezaji wazawa na kigeni.

Walter alisema kuwa ushindani umetokana na ujio wa Kocha mpya Miguel Gamondi, kila mchezaji kupambana kumshawishi kocha ili aingie katika kikosi hicho.

Aliongeza kuwa wachezaji ambao hawakuwa sehemu ya kikosi cha kwanza katika msimu uliopita baadhi Denis Nkane na Chrispin Ngushi nao wameonyesha ushindani mkubwa .

“Ninaamini msimu huu kazi itakuwepo ya kushindania namba katika kikosi cha kwanza kutokana na kila mchezaji kutaka kuwepo sehemu ya kikosi cha kwanza.

” Wale wachezaji wa zamani ambao msimu uliopita ndio wamefanya ushindani uwe mkubwa, kwani wanaamini watapata nafasi ya kucheza kutokana na ujio wa kocha mpya.

“Gamondi ana kibarua kigumu katika msimu ujao kwenye kupanga kikosi, kwani kila mmoja yupo katika kiwango bora,” alisema Walter.

SOMA NA HII  CHAMA NAE AONYESHWA MLANGO WA KUTOKEA MSIMBAZI..... ISHU IKO HIVI