Home news ROBERTINHO AMCHIMBA MKWARA GAMONDI BAADA YA KUMPORA NGAO YA JAMII

ROBERTINHO AMCHIMBA MKWARA GAMONDI BAADA YA KUMPORA NGAO YA JAMII

Habari za Michezo

KOCHA wa Simba Roberto Oliveira ‘Robertinho’ kabla kidonda hakijapoa ametuma salamu ya vitisho kwa watani wao Yanga akiwaambia Ngao ya jamii imetangulia tu watayatema yote.

Akizungumza na Mwanaspoti ikiwa ni siku moja tu tangu wachukue ngao ya jamii juzi kwa kuwapokonya Yanga kwa mikwaju ya penalti alisema hatua ya kwanza imekamilika kwa kulichukua taji hilo na sasa inakuja opresheni nyingine kabambe na wamedhamiria kubeba makombe yote.

Robertinho alisema ingawa haikuwa rahisi kuchukua taji hilo lakini kikosi chake kinataka kutumia morali hiyo kuanza kukimbia haraka kwenye ligi ikiwa ni hatua ya hesabu ya kuchukua mataji mengine.

“Haikuwa rahisi lakini nawapongeza wachezaji wangu hii ni mechi ya watani huwa ina ugumu wake lakini kwetu jambo kubwa tumechukua hili taji la kwanza na safari inayofuata ni kuanza kuyasaka mengine,” alisema.

“Unapoanza kuanza msimu na mafanikio kama haya kuna morali kubwa inajengeka kwenye mioyo yetu, nimekuta klabu hii ina miaka miwili bila taji kwa hadhi ya Simba haikuwa sawa sasa tunaingia kwenye ligi tukiwa na nguvu kubwa.

“Mimi ni kocha ambaye kote nilikopita nimekuwa natamani kuchukua mataji na nimekuwa nayapata, bahati mbaya hapa mwaka wa kwanza sikupata kombe lolote na kulikuwa na sababu na huu ni mwanzo.

Robertinho alikiri kuwa kikosi chake hakikucheza vizuri kwenye mchezo huo hasa kipindi cha kwanza akiutaja uwanja kwamba uliwazuia kucheza mpira wao wa samba lakini pia muunganiko wa wachezaji wake.

“Nimeona watu wanasema hawajafurahi, nikweli najua mashabiki wa Simba wanataka kuiona timu yao inacheza mchezo wa kuvutia lakini ilikuwa ngumu kucheza soka la aina ile kwenye uwanja wa namna ile.

“Hatukucheza vizuri kweli kipindi cha kwanza nikasema kipindi cha pili tubadilike kutoka ule mfumo wa 4-2-3-1 kuja 4-3-3 ambao kwa kiasi ulitufanya tuwadhibiti wapinzani wetu.

“Kila kitu kinakwenda kwa nafasi yake kwa uwanja ule kitu cha kwanza na bora ilikuwa kuchukua taji lakini sasa tunarudi kuendelea kuwaunganisha wachezaji nilisema tunahitaji siku zisipungua kumi na tano kuanza kuona Simba iliyokamilika na kucheza kama tunavyotaka.”

SOMA NA HII  GAMONDI AFUNGUKA HAYA KUHUSU MCHEZO WAO NA SINGIDA FG