Habari za Simba
Habari za michezo

SIMBA WANAJAMBO LAO LEO, KIVUMBI LIGI KUU

Staff Desk August 17, 2023 12:34 pm

MIAMBA ya soka nchini Simba, leo inaanza kampeni ya kusaka ubingwa wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mchezo huo pekee leo wa ligi hiyo utafanyika kwenye uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoa wa Morogoro.

Ligi hiyo imeshuhudia michezo miwili Agosti 16, Azam ikiifunga Tabora United mabao 4-0 na Mashujaa ikiichapa Kagera Sugar mabao 2-0.

Hata hivyo, mchezo wa Azam na Tabora United ulishindwa kuendelea baada ya wachezaji wawili wa Tabora UTD kuumia na kufanya wabakie sita uwanjani na hivyo mchezo kukosa sifa kikanuni kuendelea.

MTIHANI WA ROBERTINHO…… HAFIDHI ,MUSONDA WAWEKWA KIKAO KAMA UTANI MZAMIRU ABEBWA NA PENATI ZA NGAO YA JAMII

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply