Habari za Yanga
Habari za michezo

ISHU YA AUCHO IKO HIVI UKO CAF

Staff Desk August 19, 2023 12:46 pm

Unaweza kusema kiungo Khalid Aucho ameanza na gia kubwa msimu huu. Kiungo huyo wa Kimataifa kutoka Uganda alin’gara katika kikosi cha Yanga kwenye mechi mbili za Ngao ya Jamii mkoani Tanga.

Msimu uliopita alikuwa chaguo la kwanza kwa Kocha Nasreddine Nabi katika eneo la kiungo na mapema tu msimu huu amekuwa chaguo la kwanza kwa Miguel Gamondi.

Pamoja na ubora wa wachezaji waliosajiliwa na Yanga katika eneo la kiungo, Aucho ameendelea kuwa na ‘kiti cha kudumu’ katika kikosi cha kwanza.

Habari njema ni kuwa adhabu yake ya kufungiwa mechi mbili na CAF ilimalizika baada ya kukosa mechi zote za fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya USM Alger msimu uliopita.

Hakuna shaka Jumapili atakuwepo uwanja wa Azam Complex katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya ASAS Fc.

DOUMBIA KUMBE HAJAMALIZANA NA YANGA, ISHU IKO HIVI SIMBA WAPATA PIGO…. KRAMO MAMBO SIO MAMBO, DAKTARI AANIKA UKWELI WOTE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply