Tetesi za usajili wa Simba
Habari za michezo

SIMBA WAPATA PIGO…. KRAMO MAMBO SIO MAMBO, DAKTARI AANIKA UKWELI WOTE

Staff Desk August 19, 2023 1:59 pm

Kutokana na sintofahamu iliyoibuka juu ya wapi alipo winga wa Simba, Aubin Kramo raia wa Ivory Coast, ambaye tangu amesajiliwa na Simba, hajacheza mechi hata moja licha ya kuonekana kwenye benchi katika mechi kadhaa ikiwemo dhidi ya Power Dynamos na ile ya Yanga SC ya Ngao ya Jamii, uongozi wa Simba umefunguka.

Daktari wa Simba, Edwin Kagabo anasema; “Aubin Kramo hajaonekana kwenye mechi tatu na hiyo inatokana na changamoto aliyopata kwenye mazoezi ya mwisho wakati tukijiandaa na mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate FC.

“Kwa bahati mbaya goti lake lili-twist’ vibaya na kupata changamoto ya ligament ambazo zinaweka stability kwenye goti, baada ya uchunguzi na vipimo ambavyo tumevifanya tumegundua jeraha lake sio kubwa sana.

“Timu ya madaktari tukampa mapumziko na ku-focus na matibabu lengo kuu likiwa ni kuondoa hatari ambayo ingeweza kusababisha kuumia zaidi na kukaa muda mrefu nje.

“Anaendelea vizuri na ameshamaliza matibabu awamu ya kwanza ya awamu na ya pili kwa hiyo leo tutakuwanae kwenye mazoezi tukiendelea kumfanyia ufatiliaji kuona hali yake ikoje,” amesems Dkt. Edwin Kagabo.

ISHU YA AUCHO IKO HIVI UKO CAF KWA HILI GAMONDI LAZIMA AKUNR KICHWA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply