Habari za Yanga SC
Habari za michezo

SKUDU ATIMKA YANGA, UONGOZI WAFUNGUKA…. ISHU IKO HIVI

Staff Desk August 19, 2023 10:58 am

Klabu ya Yanga imethibitisha kuwa winga wake Mahlatse Makudubela ‘Skudu’ ameondoka nchini jana kurudi kwao Afrika Kusini kwa ajili ya kushughulikia zoezi la kupata hati mpya ya kusafiria.

Skudu amepata ruhusa hii ya benchi la ufundi la klabu hiyo kwenda kushughulikia jambo hilo mapema kabla mechi za Kimataifa hazijachanganya na Klabu ikakosa kumtumia.

“Skudu aliumia tulipokuwa Tanga, lakini tayari alishaanza mazoezi mepesi kurejea kwenye timu. Kocha akaona ampe ruhusa muda huu kwenda kushughulikia hati yake ya kusafiria ili kukwepa usumbufu wa safari baadae.

“Hati yake ya kusafiria ya sasa hivi inaelekea kujaa hivyo kumpa nafasi ya kupumzika kupona vizuri amepewa na ruhusa ya kusafiri kulimaliza na jambo hili la hati ya kusafiria haraka,” alisema Meneja wa kikosi cha klabu hiyo Walter Harrison.

Skudu anatarajia kurejea nchini tarehe 24 kujiunga na kikosi kuelekea mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya ASAS kutoka Djibout.

SHIDA NI MZAMIRU….. ROBERTINHO AMTANGA INGONGA SIMBA, JULIO AFICHUA UKWELI AHMED ALLY ACHAFUKWA AFUNGUKA MAZITO KUHUSU SIMBA MBOVU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply