Goli la Mayele
Habari za michezo

HATIM AWASHAURI JAMBO HILI YANGA UPANDE WA KOCHA

Staff Desk August 21, 2023 12:07 pm

Mchambuzi wa soka, Haatim Abdul amesema Yanga SC wanahitaji mwalimu wa wafungaji kwani wanapata nafasi nyingi lakini wanashindwa kuzitumia.

Amesema, Yanga wanatakiwa kumtafuta mwalimu anayeweza kuwaelekeza mbinu za kufunga kwani kwa kiasi kikubwa wanafanya kila kitu kwenye mchezo lakini unakosekana umakini kwenye eneo la ufungaji.

“Wanamiliki vizuri mpira katikati, wanacheza kuanzia golini kwao lakini kule mwishoni bado kunakuwa na shida, wakati fulani Orlando Pirates walikuwa na tatizo kama hili, wakamtafuta kocha wa wafungaji wakamaliza tatizo hilo ndani ya muda mfupi,” alisema Haatim.

Yanga jana walicheza na ASAS ya Djibouti mchezo wa hatua ya kwanza ya Klabu Bingwa Afrika na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa 2-0 lakini walipoteza nafasi nyingi za wazi.

SIMBA GARI LIMEWAKA, PHIRI AANZA KUTUPIA, BALEKE KAMA KAWA SIMBA HATA WAONGEZA POINTI KIASI GANI, YANGA ITAWASHUSHA TU. KAMWE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply