Home Habari za michezo KUHUSU UWEZO WA CHE MALONE NA MASTAA WAPYA SIMBA…MSIMAMO WA ROBERTINHO HUU...

KUHUSU UWEZO WA CHE MALONE NA MASTAA WAPYA SIMBA…MSIMAMO WA ROBERTINHO HUU HAPA…

Habari za Simba

Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Oliveira ‘Robertinho, kuweka wazi siri ya wachezaji wake wapya wa kimataifa ambao wameanza kuonesha makeke katika Michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2023/24.

Juzi Jumapili (Agosti 20), Simba SC iliibuka na ushindi wa 2-0 katika mchezo wa mzunguuko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam ikiwa ni siku chache baada kuitandika Mtibwa Sugar kwa mabao 4-2, katika mechi ya awali msimu huu.

Kocha Robertinho, amesema nyota wapya wa kimataifa waliosajiliwa msimu huu wanahitaji muda kabla ya kuanza kuonyesha uwezo.

Wachezaji hao ni beki wa kati, Che Fondoh Malone Junior kutoka Coton Sport ya Cameroon, winga wa kushoto, Aubin Kramo Kouame kutoka ASEC Mimosas ya vory Coast na mshambuliaji Mcameroon, Leandre Essomba Willy Onana kutoka Rayon Sport ya Rwanda.

Kocha huyo amesema wachezaji hao bado hawajazoea mazingira, kuelewana na wenzao na ndio maana wameshindwa kuonyesha viwango vinavyyotarajiwa.

“Wachezaji hao wana viwango vizuri lakini warnahitaji muda zaidi wa kufanya kile ambacho benchi la ufundi na mashabiki tunataka kukiona, si mwanzo mbaya lakini bado wanapaswa kufanya vizuri zaidi,” amesema.

Hata hivyo, Kocha huyo raia wa Brazil amesema, anafurahi kuiona timu yake ikifanya mashambulizi na kumiliki mchezo kwa asilimia kubwa.

Katika hatua nyingine ,Winga wa Simba SC, Aubin Kramo anamalizia muda wake wa mapumziko Ijumaa hii Agosti 25, 2023 na Jumamosi anarejea kikosini kujiunga na wenzake.

Akizungumzia suala hilo leo Agosti 23, 2023, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema Kramo alipewa wiki moja, hadi kufika Ijumaa atakuwa amekamilisha.

“Kuanzia Jumamosi atawa sawa kurudi kwenye Uwanja wa mazoezi,” alisema Ahmed.

Hata hivyo, kuna taarifa kuwa Simba wamepewa mapumziko baada ya kucheza na Dodoma Jiji FC, watarejea kambini Jumapili hii Agosti 27, 2023.

SOMA NA HII  AHMED ALLY:- MSIMU ULIOPITA TUMECHEZEWA SANA...