Home Habari za michezo AUCHO, AZIZ KI NA MUDATHIRI WATENGENEZA ‘BOMU’ YANGA….

AUCHO, AZIZ KI NA MUDATHIRI WATENGENEZA ‘BOMU’ YANGA….

Habari za Yanga

VIUNGO watatu wa Yanga, Khalid Aucho, Mudathir Yahya pamoja na Stephane Aziz Ki, wametengeneza pacha moja matata sana ambayo imekuwa ikiwapatia ushindi Wanajangwani hao katika michezo mbalimbali.

Hiyo inadhihirishwa na ushindi wa mabao 5-0 walioupata Wanajangwani hao mbele ya KMC mchezo wa kwanza wa Yanga wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa jana usiku katika dimba la Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Wachezaji hao watatu katika nafasi hiyo ya kiungo, walionekana kuelewana sana kiasi cha kumfanya Kocha Mkuu wa kikosi hicho Miguel Gamondi kutamka wazi kwamba, anao vijana wanaoijua shughuli katikati ya Uwanja.

Wachezaji hao pia walionyesha uelewano mkubwa michezo iliyopita ikiwamo ule wa nusu fainali Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc waliibuka na ushindi wa mabao 2-0, yaliyofungwa na Aziz Ki pamoja na kinda Clement Mzize.

Hata katika mchezo wa fainali dhidi ya Watanzani zao wa jadi Simba, Ngao ya Jamii michezo ambayo yote ilichezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, wachezaji hao walionyesha uelewano mzuri licha ya kupoteza kwa mikwaju ya penati 3-1.

Mbali na michezo hiyo ya hapa nyumbani, watatu hao pia waliokiwasha vilivyo katika mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASA kutona nchini Djibouti mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex mwishoni mwa wiki iliyopita Wanajangwani hao wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Akizungumzia uwezo wa nyota hao mara baada ya kukamilika kwa dakika 90 kwa mchezo wa ligi kuu didi ya KMC FC, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi alisema hiyo ni kutokana na namna wanavyojituma kuanzia kwenye Uwanja wa mazoezi huku akitamka wazi kuwa, anatarajia wachezaji hao kwamba watakuwa chachu ya mafanikio msimu huu.

Alisema mchezo ulikuwa mzuri anawapongeza wachezaji walivyopambana, ule ndio mchezo anaoutaka kuona kwenye timu yake ikicgeza vile katika michezo yote iliyopo mbele yao hadi mwisho wa msimu.

“Tumekuwa tukifanya mazoezi makali ili kuiweka Yanga katika kiwango kizuri na kuwapa furaha mashabiki na leo (juzi) wamefurahi kuona tumetawala mchezo na kupata ushundi mzuri.

Bado mimi na wenzangu tunaisuka Yanga ili iwe ile tunayofikiria nankuwa bora zaidi, tutaendelea kufanyia kazi makosa ya mechi baada ya mechi ili tuwe bora zaidi,” alisema Gamondi.

SOMA NA HII  ISHU YA FEI TOTO YAPAMBA MOTO...CHAMA CHA WACHEZAJI KIMEINGILIA KATI