Home Habari za michezo KUHUSU MSUVA KURUDI YANGA UKWELI WOTE HUU HAPA….TFF WAIPA NAFASI SIMBA….

KUHUSU MSUVA KURUDI YANGA UKWELI WOTE HUU HAPA….TFF WAIPA NAFASI SIMBA….

Habari za Michezo

KUNA hesabu ngumu mabosi wa Yanga wanazipiga juu ya kukiboresha kikosi chao hasa juu ya kuiongezea makali safu yao ya ushambuliaji na kuna mastraika watatu wanaumiza vichwa vya vigogo wa timu hiyo huku jina la Simon Msuva likirejea mezani.

Yanga inafikiria kurudi sokoni baada ya kununua mtu wa haraka wa kuwafungia mabao baada ya Kocha Miguel Gamondi kugundua kwamba washambuliaji wanne alionao wanahitaji muda zaidi kumpa anachotaka.

Hesabu za mabosi wa Yanga ni baada ya kuisoma timu yao na kujadiliana pia na Gamondi baada ya kucheza mechi mbili za ngao ya jamii zilizopigwa pale Mkoani Tanga.

Kitendo cha timu yao kuutawala mchezo dhidi ya Simba wakishindwa kuamua kwa makali ya washambuliaji wao wakiwatumia watatu kati ya hao wanne Clement Mzize na Kennedy Musonda walioanza huku Hafiz Konkoni akiingia wakishindwa kuipasua ngome ya watani,kumewapa ujumbe tosha vigogo kwamba wanahitaji kununua mtu wa kazi.

Yanga haraka wakaanza hesabu za kusaka mshambuliaji mpya atakayekuja kusaidiana na hao wanne huku mezani kwao kukiwa na washambuliaji Mkongomani Makabi Lilepo wa Al Hilal, Simon Msuva na George Mpole.

Yanga wanajua kwamba endapo hata watakubaliana na Al Hilal ambao wameweka ngumu wakionekana kama wanakunja wakidai walinyimwa Fiston Mayele ambaye aliuzwa Pyramids ya Misri bado kuna ugumu.

Ugumu wa usajili wa Lilepo ni kwamba, utailazimisha Yanga kuondoa jina moja la mchezaji wa kigeni kati ya nyota 12 walipo ikiwa idadi kamili ya kikanuni kwa wageni hao.

Lakini kumuondoa mtu huyo kunamaanisha kuna gharama ya kumlipa pia vinginevyo waingie kwenye kesi na Fifa.

Hesabu za pili kwa Yanga ni kumsaka mshambuliaji mzawa na tayari walishamvutia waya George Mpole ambaye ni mali ya FC Lupopo ya DR Congo akawaambia yuko freshi ni wao tu.

Sasa mabosi wa Yanga bado wanafikiria jinsi ya kuongea na rais wa klabu hiyo Jacques Kyabula ambaye anamkubali sana mshambuliaji huyo.

Lakini yote kwa yote karata kubwa ya Yanga na inayowaumiza kichwa zaidi ni Simon Msuva. Wanapiga hesabu za jinsi gani ya kumshawishi kiutu uzima arudi nyumbani.

Yanga inajua msimamo wa Msuva anayetaka kuendelea kucheza nje akiwahi kuliambia gazeti la Mwanaspoti kuwa anaweza kuja kurejea klabu yake hiyo iliyomuuza nje kwa mara ya kwanza lakini sio kwasasa.

Hata hivyo msimamo huo ni kama haujaeleweka kwa mabosi wa Yanga na  juzi walikuwa wanamjadili Msuva wakiangalia uwezekano wa kumchukua haraka.

Msuva kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu yake ya Saudi Arabia ya Alqadisiah.

TFF yatoa ufafanuzi

Nafasi ya Yanga kusajili mshambuliaji inaweza kubaki kwa kumsajili Msuva pekee na endapo itatoa sababu za kutosha zitakazowaridhisha Shirikisho la Soka Afrika (CAF) wanaoweza kumchomeka kwa faini.

Yanga dirisha la usajili sambamba na Azam na Singida Fountain Gate lilishafungwa ambapo kama Yanga itamsajili Msuva anaweza kuingia endapo tu watatoa sababu, huku pia hatua ya mshambuliaji huyo kuwa huru ikiwarahisishia kwa kuwa bado dirisha la ndani la usajili halijafungwa.

Usajili wa ndani utafungwa Agosti 31 saa 6:00 usiku Msuva anaweza kuingia kabla ya muda huo kumalizika.

Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi ameliambia Mwanaspoti kuwa kwasasa ni Simba pekee ambao ndio wanaweza kufanya usajili huku klabu zingine muda wao umemalizika na labda kuwe na sababu kubwa itakayowaridhisha CAF.

“Simba pekee ndio wanaweza kusajili sasa bila kikwazo, na sababu zao ni mbili kwanza ni kutokana na hatua yao ya kuanzia hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika na sababu ya pili ni hiyo ya ushiriki wao wa Super Cup,”alisema Madadi ambaye kocha wa zamani wa Taifa Stars.

“Klabu zingine zinaweza kusajili lakini hapo wanaweza kukutana na malipo ya adhabu lakini kikubwa hapa ni kama hiyo klabu itatoa sababu nzito ambayo CAF itawaridhisha na kuwapa hiyo nafasi.

SOMA NA HII  BAADA YA KUPOTENA NA SIMBA..., MKUDE KUKAKABIDHIWA SHUGHULI ZA KANOUTE LEO..