Habari za Simba leo
Habari za michezo

SIMBA MSIMU HUU HAITAKI KUFUNGWA, VIONGOZI WAJA NA HILI

Staff Desk August 25, 2023 1:57 pm

Uongozi wa Simba SC umeweka wazi kuwa, malengo yao msimu huu ni kushinda mechi zote watakazocheza kwenye Ligi Kuu na mashindano mengine, huku wakiweka rekodi ya kuwa timu isiyofungika.

Baada ya kupoteza taji la Ngao ya Jamii, Young Africans ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu wakibeba mara mbili wameweka wazi kuwą malengo yao msimu huu ni kuhakikisha wanatetea mataji yote ambayo walibeba msimu uliopita na wanaendelea kuyashikilia.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema, watashinda mabao mengi kwenye kila mchezo na hawataruhusu bao lolote kwenye mechi hizo zinazofuata.

“Tunasikitika kuwa, tumecheza mechi mbili za ligi mpaka sasa na kufunga mabao sita tu na kuruhusu mabao mawili. Hili ni jambo ambalo hatuwezi kulifurahia.

“Kwa namna ambavyo timu yetu ilivyo na wachezaji bora na wakali zaidi Barani Afrika, ilipaswa tuwe tumefunga mabao mengi sana na kutoruhusu bao lolote.

“Tumeshinda mabao sita na kuruhusu mawili. Kocha wetu na wasaidizi wake, wanakwenda kurekebisha hilo, tunataka kuwa klabu iliyofunga mabao mengi na kufungwa mabao machache,” amesema Ahmed.

Simba SC waliwachapa Mtibwa Sugar 4-2 pale Manungu Morogoro kwenye mchezo wa kwanza na kisha kuwachapa Dodoma Jiji FC mabao 2-0 kwenye mechi ya pili iliyochezwa Uwanja wa Uhuru.

LIPWA MPAKA MARA 1000 YA DAU LAKO KWA KILA USHINDI WA SLOT YA FOXPOT…. KUELEKEA MECHI YA KESHO YA CAF….GAMONDI AFUNGUKA ATAKAVYOIMALIZA KAZI MAPEMA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply