Home Habari za michezo NABI NA YANGA NI JINO KWA JINO CAF…ISHU NZIMA IKO HIVI….

NABI NA YANGA NI JINO KWA JINO CAF…ISHU NZIMA IKO HIVI….

Habari za Yanga SC

Wakati Yanga ikifuzu kwa jeuri hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikitupa nje ASAS ya Djibouti kocha wao wa zamani Nasreddine Nabi naye amepita njia hiyohiyo kibabe.

Yanga imewatupa nje ASAS kwa ushindi wa jumla wa mabao 7-1 wakitangulia kushinda mechi ya kwenda kwa mabao 2-0 kisha jana kumaliza kibabe mchezo wa pili kwa mabao 5-1.

Nabi ambaye kwasasa anaifundisha FAR Rabat ya ambao ni mabingwa wa Morocco naye akitangulia kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 ugenini nchini Togo dhidi ya ASKO Kara ya huko kisha kushinda nyumbani kwa mabao 7-0 Jana usiku.

Yanga kwenye ushindi huo imetoa mwamba mmoja Maxi Nzengeli aliyeweka kambani mabao mawili kwenye mchezo wa pili dakika wakati Nabi ametoa mastaa watatu waliofunga mabao kama hayo.

Kwenye ushindi wa Jana washambuliaji Lamine Diakite aliyefunga mara moja kwenye kila mchezo,Ahmed Hammoudan beki Anour Tarkhatt wote walifunga mara mbili timu yao ikifuzu.

Wapinzani wajao wa Yanga El Merreikh wameanza harakati za kutaka kuuhamisha mchezo huo ufanyike nchini Morocco kutoka Rwanda walikocheza mechi yao kwanza ambapo endapo watafanikiwa wanaweza kuifanya Yanga kupishana na Nabi.

Endapo Shirikisho la Soka Afrika CAF itabariki maombi ya Merreikh na Yanga ikisafiri kwenda Morocco Septemba 15 watajikuta wanapishana na Nabi ambaye atakuwa nchini Tunisia kukutana na Etoile du Sahel kwenye mchezo wa kwanza.

Nabi atarudi nyumbani Septemba 29 wakati Yanga ikiwa nyumbani siku hiyo kumalizana na Merreikh wote wakiwania kutinga makundi.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO NBC PREMIER LEAGUE ILIVYOMALIZIKA KWA REKODI ZA KIBABE...