Mashabiki wa Simba SC kiroho safi wameomba Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania {TFF} ikiwezekana waufungie uwanja wa Azam Complex ili Yanga warudi kwenye uwanja wa Uhuru kutokana na kupata matokeo kila mechi kwenye uwanja wa Azam Complex.
Mashabiki hao wamesema hilo baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kumalizika jana na Yanga kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 5-0 dhidi ya JKT ikiwa ni mchezo wa tatu mfululizo Yanga ikishinda kwa bao 5 kila mechi.
โSisi hatuvutiwi namna ambavyo yanga inacheza isipokuwa kwa sababu tunapenda mpira hatuwezi kusema uongo wakati kitu kinaonekana. Nilisema unaweza kuidharau Yanga lakini hii ndiyo yanga bora kabisa kuwahi kutokea, haimtegemei mchezaji mmoja kama msimu uliopita walikuwa wakimtegemea Mayele pekee.
โHii Yanga ni hatari, nilisema JKT huenda akapigwa tano na kweli amefungwa tano, ninaumia na sipendi Yanga afunge bao 5 lakini ndiyo inatokea.
โNina ombi kwa TFF, kama inawezekana huu Uwanja wa Azam Complex waufungie, Yanga arudi Uwanja wa Uhuru kwa sababu hivi vitu vinavyotokea ni madhara makubwa na inaonyesha Azam FC wameshindwa kuutumia uwanja wao wa nyumbani, Yanga wanaumiliki huu uwanja, kwenye siku 9 wamefunga mabao 15,โ wamesema mashabiki hao.