Habari za Yanga leo
Habari za michezo

NABI AITABIRIA MAKUBWA YANGA YA GAMONDI

Staff Desk August 31, 2023 11:25 am

Kocha wa zamani wa Yanga, Nassredine Nabi amesema kuwa ameiangalia Yanga ya sasa chini ya Miguel Gamondi na kusema kuwa inauwezo mzuri wa kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

Nabi kwa sasa ni kocha wa Far Rabat ya Morroco na msimu uliopita aliiongoza Yanga kuipa ubingwa wa ligi kuu, Kombe la FA Ngao ya Jamii na kufika fainali katika Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ni rekodi kwa timu hiyo.

Akizungumza kuhusiana na uwezo wa Yanga kutwaa ubingwa msimu huu, Kocha Nabi alisema kuwa bado anaamini Yanga wana timu nzuri baada ya kuiangalia katika michezo kadhaa ambayo wamecheza mpaka sasa na kubaini kuwa bado wanakikosi imara.

“Yanga bado wana timu nzuri na tayari nimeona michezo kadhaa ambayo wamecheza, usajili ambao umefanyika ni mzuri na mara zote wamekuwa na machaguo sahihi, uongozi ulikuwa makini katika hilo.

“Ambacho kipo kwa sasa ni kwa kocha kuona namna gani ataweza kuwatumia wachezaji na kupata matokeo, kuwaunganisha vyema na kujua jinsi ya kuwatumia katika michezo husika,” amesema kocha huyo.

PHIRI AFUNGUKA KILA KITU KUHUSU UGOMVI WAKE NA ROBERTINHO, ISHU IKO HIVI KWA HILI YANGA HII IMESHAKUWA BALAA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply