Home Habari za michezo AMBANGILE AWEKA WAZI UHATARI WA YANGA KWENYE MASHAMBULIZI

AMBANGILE AWEKA WAZI UHATARI WA YANGA KWENYE MASHAMBULIZI

Habari za Yanga

Mchambuzi maarufu wa masuala ya soka nchini Tanzania, George Ambangile amesema kuwa kikosi cha Yanga Sc chini ya kocha wao, Miguel Gamondi ni hatari zaidi wakiwa wanashambulia jambo ambalo linawafanya wapinzani wao wanapocheza nao kupata wakati mgumu namna ya kuwadhibiti.

Ambangile amesema hayo wakati akizungumzia kikosi cha yanga msimu huu kutokana na moto wanaoendelea kuuwasha baada ya kufunga bao 10 katika mechi mbili za kimashindano walizocheza hivi karibuni.

“Kwa jinsi Yanga wanavyocheza, msingi wao mkubwa upo kwenye kuzuia, mpaka umfikie Diarra lazima uwe umefanya kazi kubwa sana. Sasa hivi wameongeza sumu nyingine ya kutumia nafasi zao wanazotengeneza.

“Ukiangalia timu Gamondi hajampa mchezaji nafasi ya moja kwa moja, unaweza kushangaa leo umecheza vizuri na kesho ukapigwa benchi, anataka kila mchezaji aheshimu jezi ya yanga. Ukitazama mchezaji anayeanza na anayeingia unasema mambo ni yaleyale.

“Yanga wanapokwenda kushambulia ni hatari zaidi, msimu uliopita walikuwa wanamtegema Mayele pekee, sasa hivi movements ni nyingi sana, idadi ya wachezaji wanaofika kwenye penalty box la mpinzani ni wengi sana, tena wengi wao wanakuwa ni viungo. Mudathir, Aziz, Maxi, pacome wote wanafika kwenye penalty box ya mpinzani.

“Gamondi ameweka mfumo wa kiuchezaji na ndani ya huo mfumo kuna uhuru, ukiangalia kwenye karatasi utaona ni kama 4-2-3-1, lakini jinsi wanavyoanza kucheza unaona viungo wa kati wawili wanakuwa wapi, Yanga wanatembea sana wakifika mbele.

“Yanga wakiupoteza mpira kila mtu atafanya kazi kubwa kuurejesha ule mpira kwenye himaya yao kuanzia huko huko kwa mpinzani. Gamondi hapendi mpinzani akae na mpira muda mrefu,” amesema Ambangile.

SOMA NA HII  MAXI APEWA KAZI MPYA YANGA...GAMONDI AKITANGAZA VITA MPYA AFRIKA...