Home Habari za michezo BAADA YA ‘KUWABATUA’ WADJIBOUT JANA…MPANGO MPYA WA GAMOND UKO HIVI….

BAADA YA ‘KUWABATUA’ WADJIBOUT JANA…MPANGO MPYA WA GAMOND UKO HIVI….

Habari za Yanga SC

BAADA ya kufanikiwa kusonga mbele katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Angel Gamondi amesema sasa muda wa kufanya maandalizi ya mchezo uliopo mbele yao dhidi ya El Mareikh ya Sudan.

Yanga juzi ilifanikiwa kusonga mbele baada ya kushinda mabao 5-1 dhidi ya As Al Sabieh (Asas FC) kutoka Djibouti, kwenye uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Max Nzengeli dakika 7,90, Hafiz Konkoni (dakika 45), Pacome Zouzoua (dakika 55) na Clement Mzize (dakika 69), bao la Asas FC limefungwa na Tito Mayor kwa penalti dakika ya 85.

Kwa matokeo hayo Yanga imeibuka na jumla ya mabao 7-1 na wanatarajia kukutana na El Mareikh ya Sudan, mchezo wa kwanza Yanga watakuwa nyumbani na marudiano utaenda kuchezwa Rwanda ambalo wapinzani wao wamechangua nchi hiyo kutumia uwanja wa nyumbani .

Akizungumza mara baada ya 90 kukamilika, Gamondi alisema wanatumia siku moja kusherehekea ushindi wa dhidi ya Asas FC baada ya hapo watakuwa na kazi kubwa ya kujiandaa na mechi yao ijayo na El Mareikh.

Alisema anaifahamua El Mareikh ni timu kubwa na wanaozoufu wa mashindano hayo wanatakiwa kufanya maandalizi mazuri ya kutafuta ushundi mechi ya nyumbani na baadae kumaliza ugenini.

“Tumemaliza hatua hii tumesonga mbele, lakini tuna kazi kubwa mbele yetu kushinda mechi zote mbili na kutinga hatua ya robo fainali, tunaenda kufanyia kazi mapungufu yaliyijitokeza katika mechi yetu ya leo (juzi).

Tumecheza vizuri lakini kama benchi la ufundi kuna mapungufu nimeyaona na naenda kuyafanyia kazi kukisuka kikosi na kuwa imara zaidi ya sasa,” alisema Gamondi.

Kuhusu mechi iliyopia na Asas FC, Gamondi alisema amefurahishwa na jinsi walivyocheza wachezaji wake, kufanyia kazi kile alichoelekeza kwenye uwanja wa mazoezi.

Alisema walicheza kwa umakini mkubwa ikiwemo safu ya ushambuliji, kiungo na hata ulinzi lakini hakufurahishwa na kitengo cha Zawadi (Mauya) kwa kucheza rafu anbayo ilisababisha penalti.

“Ni kweli sikupenda kitendo kile alichokifabya Mauya, nilimueleza mara kwa mara hata tunapokuwa kwenye mazoezi human ya makosa kama haya anbayo imetugharibu na kuruhusu kufungwa bao kwa penalti,” alusema kocha huyo na aliongeza kuwa:

Anatengeneza timu kwa kila mchezaji awe na uwezo wa kufunga, pia kucheza mpira mzuri ambapo utawasaidia mbeleni katika mashindano au mechi zilizopo mbele yao,” alisema Gamondi.

Naye kiungo mshambuliajiwa timu hiyo, Max Pia Nzengeli alisema anafurahi kuona viongozi wa Yanga kumpa thamani kwa siku ya juzi kuipa ni siku yake kwa kuipa jina la Max Day.

Alisema hiyo ni ishara kubwa ya upendo kwa uongozi na mashabiki na kuhakikisha kuwa ataheshimu upendo huo na kupambania timu hiyo inafikia malengo yao ikiwemo kucheza makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo kwa miaka mingi Yanga haijawahi kufika hatua hiyo.

Kocha wa Asas FC, Muwlid Ali Beilleh alisema walishindwa kutimiza mipango yao baada ya kufanya makosa na Yanga kuyatumia na kuruhusu idadi kubwa ya mabao.

Alisema mechi hii waliingia kwa kufunguka kufanya mashambulizi tofauti na mechi ya kwanza ambayo waliruhusu bao 2-0, walicheza kwa kuzuia zaidi.

“Tumekubali matokeo, niwapongeze wachezaji wangu kupambana na timu kubwa ambayo imecheza mpira mzuri na kufanikiwa kupata ushindi, katika mpira kuna mambo matatu, kufungwa, kushinda na sare, tumekubalu kupoteza na tunaenda kujipanga kwa msimu mwingine,” alisema Ali Beilleh.

SOMA NA HII  KUHUSU KUFUNGA SANA MAGOLI .....MUDATHIR HUYU HAPA....AANIKA KILICHONYUMA YAKE...