Home Habari za michezo SIMBA WATAMBA KUTANGAZA UBINGWA KABLA YA MECHI TANO, VIGOGO WATEMA CHECHE

SIMBA WATAMBA KUTANGAZA UBINGWA KABLA YA MECHI TANO, VIGOGO WATEMA CHECHE

Tetesi za Usajili Simba

SALIM Abdallah ‘Try Again’ ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba amewaambia mashabiki wa Simba kuwa wajiandae kufurahia msimu ujao kwa kuanzia ‘Simba Day’ huku akitamba kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu Bara wakiwa wamebakisha michezo mitano mkononi.

Kauli hiyo aliitoa wakati wakiwa katika maandalizi ya Tamasha la Simba Day litakalofanyika Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika tamasha hilo, Simba inatarajiwa kucheza mchezo maalum wa kirafiki dhidi ya Power Dynamos ya nchini Zambia sambamba na utambulisho wa wachezaji wake wapya na benchi la ufundi.

Akizungumza , Abdallah alisema kuwa, burudani kubwa wataanza kuipata mashabiki wa Simba kwa kuanzia mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Power Dynamos katika tamasha la Simba Day.

Abdallah aliongeza kuwa burudani hiyo wataipata kutoka kwa wachezaji wao wapya ambao wamewasajili baadhi ni Willy Onana, Fabrice Ngoma, Aubin Kramo na Fondoh Che Malone.

Aliongeza kuwa msimu ujao wamepanga kufanya vema na kikubwa ni kuhakikisha wanautangaza ubingwa mapema kabla ligi haijamalizika ya msimu ujao.

“Kwa usajili huu ambao Simba tumeufanya, basi naamini msimu ujao tutabeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara kabla ya mechi tano za mwisho, yaani tukiwa na mechi tano mkononi.

“Usajili wetu tuliofanya umeendana na mahitaji na mapendekezo ya kocha ambayo ameyafanya kwa kuwasajili wachezaji aliowahitaji.

“Hivyo mashabiki wa Simba wajiandae kufurahi msimu ujao, kwa kuanzia siku ya Simba Day Jumapili hii na kuendelea hadi katika Ngao ya Jamii,” alisema Abdallah.

SOMA NA HII  ROBERTINHO HANA WASI NA ZAMBIA, AWATUMIA WAMBA HAWA KUMALIZA KAZI