Home Habari za michezo SIMBA YAMTAMBULISHA KIPA WAKE MPYA KUTOKA MOROCCO

SIMBA YAMTAMBULISHA KIPA WAKE MPYA KUTOKA MOROCCO

ayoub

Klabu ya Simba imethibitisha kukamilisha usajili wa kipa, AYOUB LAKRED kutoka FAR Rabat ya Morocco kwa Mkataba wa miaka miwili.

Lakred (28) ameiongoza FAR Rabat kushinda ubingwa wa Ligi Kuu ya Morocco na kuifikisha Nusu fainali ya CAFCC.

Lakred anakuja Tanzania na medali ya ubingwa wa Ligi kuu ya Morocco aliyoivaa wiki kadhaa zilizopita.

Anakuja na kumbukumbu ya mwisho ya Kimataifa kwake ni kucheza robo fainali ya Kombe la Shirikisho Africa akiwa na AS Far Rabat.

Amekuja Kipa aliyekua akiitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Morocco inayocheza fainali za CHAN.

SOMA NA HII  TUCHEL AWAPIGIA SALUTI BALEKE,MAYELE..."WATAFANYA MAKUBWA CAF...AMEZUNGUMZA HAYA