Home news TFF YAFUNGUKA KUHUSU VIBALI VYA WACHEZAJI WA KIGENI WA YANGA

TFF YAFUNGUKA KUHUSU VIBALI VYA WACHEZAJI WA KIGENI WA YANGA

habari za yanga

Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ limethibitisha kupokea vibali vya wachezaji wa Kigeni wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, ikiwa ni saa chache baada ya kutoa taarifa ya kupokea vibali vya Azam FC pekee.

TFF imethibitisha kupokea vibali hivyo kwa taarifa rasmi iliyochapishwa katika vyanzo vyake vya habari, huku ikiweka wazi majina ya wachezaji 12 wa kigeni wa Young Africans waliopata vibali.

Wachezaji hao ni Djigui Diarra, Jesus Moloko, Stephane Ki Aziz, Joyce Lomalisa, Khalid Aucho, Kennedy Musonda, Koussi Yao, Gift Fred, Mahlatse Makudubela, Hafiz Konkon, Max Mpia na Zouzoua Peodoh.

Hii hapa taarifa rasmi kutoka TFFVibali yanga

SOMA NA HII  BENKI YA NBC YAZINDUA RASMI USAJILI WA MBIO ZA NBC DODOMA MARATHON 2023...