Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI ZA LIGI YA MABINGWA….SIMBA WAANGALIA PAKUJITAFUTA UPYA…

KUELEKEA MECHI ZA LIGI YA MABINGWA….SIMBA WAANGALIA PAKUJITAFUTA UPYA…

Habari za Simba

UONGOZI wa Simba upo kwenye mchakato wa kutafuta nchini jirani au ndani sehemu tulivu kwa ajili ya kwenda kuweka kambi ya muda mfupi kabla ya kucheza mechi ya kwanza ya msimu wa 2023/24 ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.

Hatua hiyo ni kuhakikisha ni kuhakikisha wanaendelea kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa ili kwenda Zambia kutafuta ushindi katika mchezo huo utakaopigwa Septema 16, mwaka huu uwanja wa Levy Mwanawasa, Ndola.

Kenya ni moja ya nchi ambayo imekuwa ikitajwa ya kwanza imeanza kujadiliwa na uingozi ili kwenda nchini humo kwa ajili ya mchezo huo.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally alisema kuelekea mchezo wa Power Dynamos wako kwenye mazungumzo na baadhi ya mataifa ya karibu ili kuona ni nchi gani tulivu kwa ajili ya kuweka kambi ya siku 12.

Alisema kati ya hizo siku 12 pia kutakuwa na mechi mbili za nguvu kutoka ndani na nje ambayo itawapa ushindani mkubwa ya kujipima kabla ya kukutana na Power Dynamos.

“Ni kweli Kenya ni nchi moja wapo ambayo imekuwa changuo la kwanza lakini pia kuna mataifa mengine ila hata Tunduma kwa sababu ni karibu, hadi sasa bado hatujajua ni wapi.

Tukifanikiwa kupata tutacheza mechi mbili za nguvu kwa mapendekezo ya benchi letu la ufundi, Roberto Oliviera (Robertinho ) kwa ajilia ya kuona uwiano wa kikosi chake kiufundi,” alisema Ahmed.

Aliongeza kuwa Power Dynamos ni timu nzuri hawataingia kwa kuwachukulia ya kawaida kwa sababu wanaamini wapinzani wao hawataingia kinyonge kwa kuwa wanahitaji kufuzu na kuingia makundi na hatimaye kucheza nusu fainali.

“Ili kuweza kukabiliana na Power Dynamos lazima tupate mechi mbili za nguvu ambazo zinampata mwanga kocha Robertinho kuona uwino wa wachezaji wake, Kikosi kimerejea mazoezi siku ya jumanane baada ya game ya Dodoma jiji tukavunja kambi na sasa timu imerejea.

Wachezaji wote wamerejea isipokuwa Ayoub Lakred ameingia leo ( jana) na kujiunga na wenzake, Nyota wawili Henock Inonga na Aubin Kramo wamerejea na ameungana na wachezaji wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Power Dynamos

Kuna maneno sio nazuri kuwa eti Kramo anapoanza mazoezi ndio anaumia, sio ukweli kwa sababu nyota huyo amecheza mechi tatu za kirafiki nchini Uturuki, baada ya kurudia tukijiandaa na Ngao ya Jamii alipata majeraha na kila akijaribu kufanya mazoezi alikuwa akihisi maumivu na jopo la madaktari alishauri apumzike kwa muda mfupi na sasa amerejea yuko fiti ni suala la kocha tu,” alisema Meneja huyo wa idara ya Habari na Mawasiliano.

Alisema Simba inaendelea na utaratibu wao wa kupeleka mashabiki nchini Zambia kwa ajili ya kwenda Ndola kushangilia timu yao, walifikiri mashabiki hao kwenda na usafiri wa treni.

“Tulifanikiwa kuzungumza nao lakini tukapata changamoto ya kurejea kwa treni kwa sababu inaondoka Septemba 12 na kurudia unatakiwa kusubiri kukaa siku mbili baada ya mechi.

Hivyo kutokana na utaratib huo tumeona bora tuendelee kutumia usajifiri wa basi letu ambapo litaondoka hapa Septemba 12 kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya kwenda kushangilia timu yao,” alisema Ahmed.

SOMA NA HII  KUELEKEA MSIMU UJAO..YANGA WAINGIA VITANI NA WAMOROCCO KUMWANIA GABADINHO..SENZO AANIKA KILA KITU...