Habari za Yanga leo
Habari za michezo

GAMONDI AMTAKA STRAIKA MWINGINE, MAMBO BADO SANA

Staff Desk September 4, 2023 2:36 pm

Yanga imeanza msimu mpya kwa kasi ikigawa dozi kwenye michuano mbalimbali inayoshiriki, lakini kama unadhani kocha Miguel Gamondi ameridhika na kasi hiyo unakosea, kwani ametoa agizo akitaka aletewe straika mmoja amalize kazi.

Ipo hivi. Licha ya Yanga kumsajili Hafiz Konkoni bado kiwango chake hakijakata kiu ya kocha wake huku akiwa ameshafunga mabao mawili kwenye kikosi hicho.

Chanzo makini ndani ya Yanga kimesema bado tu wanaendelea kutafuta mshambuliaji taratibu, ni kweli timu inashinda kwa mabao ya kutosha lakini kocha (Gamondi) anataka ufanisi zaidi wa kutumia nafasi ambazo wanatengeneza.

Kocha (Gamondi) anataka mshambuliaji ambaye kwenye nafasi tatu atafunga mbili au zote anaona timu inatengeneza nafasi zaidi ya ushindi ambao tunaupata. Hata hivyo, kwa sasa Yanga imefungiwa kusajili kutokana na kushindwa kumlipa stahiki yake, kiungo Gael Bigirimana.

Mbali na kesi hiyo, pia Yanga inakabiliwa na mtihani mwingine baada ya beki, Mamadou Doumbia aliyevunjiwa mkataba naye kukimbilia Fifa kushtaki.

KOCHA WA SIMBA HUYU HAPA TAIFA STARS….. ISHU IKO HIVI ROBERTINHO AFUNGUKA HAYA KUHUSU LUIS MIQUISSONE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply