Habari za Simba SC
Habari za michezo

ROBERTINHO AFUNGUKA HAYA KUHUSU LUIS MIQUISSONE

Staff Desk September 4, 2023 2:42 pm

Kocha Robertinho amesema amefurahishwa na kitendo cha winga Luis Miquissone kupungua uzito, akisema kurejea kwake kwenye kiwango na wepesi kutaiongezea kitu kizito timu yake huku pia akisubiri taarifa njema za kipa aliyekuwa majeruhi, Aishi Manula.

Kocha alisema Luis alirejeshwa Simba akiwa na uzito wa kilo 77, lakini hadi sasa jamaa amekata kilo nne na kubaki na 73 ambazo zimemrudisha kwenye wepesi na juzi akifunga bao lake kwenye mechi ya kirafiki ya kujipima nguvu dhidi ya Kipanga.

“Jambo zuri kuna wachezaji wetu wengine wameanza kuimarika angalia Miquissone (Luis) ni mchezaji mkubwa ambaye anajua kuamua mechi kubwa kama hizi sasa amepungua uzito anarudi kwa kasi kwenye kiwango chake, Inonga (Henock) amerejea pia tunasubiri kusikia taarifa njema kuhusu Manula (Aishi).”

GAMONDI AMTAKA STRAIKA MWINGINE, MAMBO BADO SANA SASA UNAWEZA KUSHINDA MPAKA MARA 150 YA DAU LAKO KUPITIA SLOTI HII YA KIJANJA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply